Inonga, Mayele siyo mchezo

Inonga afunguka mazito Simba

Muda mfupi kabla ya mechi kuanza beki wa kati wa Simba, Inonga Baka aliingia uwanjani na kwenda upande waliokuwa wachezaji wa Yanga (Kaskazini) kuwainua mashabiki wao na kutaka kumshangilia pamoja na timu yake.  

Inonga hakuonekana wakati timu zimepanga mistari kutoka vyumbani kuingia uwanjani na hata muda wa kusalimiana pamoja na waamuzi hakuwepo.

Wakati timu zilikuwa kwenye maeneo ya kupiga picha na kusubiri nanahodha kuchagua magoli ndio Inonga aliingia Uwanjani.

Baada ya kuingia alienda upande waliokuwa wachezaji wa Yanga na kuwainua mashabiki wao kwa kuonyesha inshara za kuwashangilia.

Mshambuliaji wa Yanga, Fiston Mayele nae wala hakuonyesha upole kwani muda huo huo aliwainua mashabiki wa Yanga kwa kutaka washangilie kama vile alivyofanya Inonga.