Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ikanga Speed yamemkuta Yanga

IKANGA Pict

Muktasari:

  • Baada ya uhakika huo, Yanga tayari wameanza kukaa mkao wa usajili wa dirisha kubwa wakiangalia zaidi maeneo ya kiungo mkabaji, beki wa kati, mshambuliaji wa mwisho, winga wa kulia anaetumia mguu wa kushoto na beki wa kulia.

LIGI Kuu Tanzania Bara ipo kwenye dakika za lala salama. Tayari nafasi nne za juu zimeshajulikana. Hiyo ikimaanisha kwamba Simba, Yanga, Azam na Singida watakwenda kimataifa msimu ujao.

Baada ya uhakika huo, Yanga tayari wameanza kukaa mkao wa usajili wa dirisha kubwa wakiangalia zaidi maeneo ya kiungo mkabaji, beki wa kati, mshambuliaji wa mwisho, winga wa kulia anaetumia mguu wa kushoto na beki wa kulia.

Mkongomani Jonathan Ikangalombo 'Ikanga Speed' huenda huu ukawa msimu wake wa mwisho ndani ya kikosi hicho. Ipo hivi; Ikangalombo aliyesajiliwa na Yanga kupitia dirisha dogo la usajili imeelezwa kuwa kutokana na kushindwa kuendana na kasi ya timu hiyo tofauti na matarajio atatolewa kwa mkopo dirisha kubwa lijalo.

Chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya Yanga kimeliambia Mwanaspoti kuwa ni kweli kuna mpango huo kutokana na mchezaji huyo kushindwa kuonyesha makali waliyokuwa wanayatarajia huku kielezwa kuwa anaweza kupelekwa Singida Black Stars.

"Ni kweli mpango huo upo na mchakato wa wapi ataenda unaendelea kufanyika muda ukifika kila kitu kitawekwa wazi mpango huo ni kutokana na mchezaji huyo kushindwa kuonyesha kile kilichokuwa kinatarajiwa na wengi licha ya kupata nafasi ya kucheza," alisema mtoa taarifa huyo na kuongeza;

"Mchakato wa kuandaa timu umeanza mapema kwa sababu ligi tayari imeisha na tunahitaji kuwa na kikosi kipana na bora msimu ujao ili tusiishie hatua ya makundi tena michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika ambayo tayari tumeshakata tiketi ya kushiriki."

Wakati chanzo hicho kikizungumzia hayo Mwanaspoti limepenyezewa habari kuwa Ikanga Speed anatolewa kwa mkopo kwenda Singida Black Stars huku Yanga wao pia wakiinasa saini ya kiungo Mohamed Damaro.

Inaelezwa kuwa makubaliano yaliyopo ni mabadilishano kati ya Ikanga Speed na kiungo huyo ambaye anacheza nafasi ya ukabaji hivyo atakuwa mbadala sahihi wa Khalid Aucho ambaye mkataba wake unamalizika mwishoni mwa msimu huu.