Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Huyo Pacome gari limewaka

New Content Item (1)
New Content Item (1)

Muktasari:

  • Pacome ambaye ni kama hakuanza msimu vizuri, hivi karibuni ameonekana kurejea katika fomu aliyokuwa nayo msimu uliopita kwa kutoa asisti na kufunga, huku akihusika kwenye mabao manane mpaka sasa katika Ligi Kuu Bara, akifunga matano na kuasisti matatu.

KIUNGO wa Yanga, Pacome Zouzoua gari limewaka, amerudi kwenye ubora wake akifunga na kufanya balaa, huku akifunguka kuwa kwa namna walivyo fiti habari ya mtu kupigwa nyingi ni kikombe ambacho kila timu inaweza kukipitia.

Pacome ambaye ni kama hakuanza msimu vizuri, hivi karibuni ameonekana kurejea katika fomu aliyokuwa nayo msimu uliopita kwa kutoa asisti na kufunga, huku akihusika kwenye mabao manane mpaka sasa katika Ligi Kuu Bara, akifunga matano na kuasisti matatu.

Kurejea kwa makali ya staa huyo kumechangiwa na mabadiliko makubwa yaliyoonekana katika kikosi hicho, kwani Yanga katika mechi nne za mwisho ilizocheza imevuna ushindi mzito wa kuanzia mabao matatu hadi matano ikizifunga timu za Mashujaa, Tanzania Prison, Dodoma Jiji na Fountain Gate.

Akizungumza na Mwanaspoti, Pacome alisema kwa namna walivyo fiti inawarahisishia kuutafuta ushindi na kufunga mabao mengi.

Alisema, anaiona Yanga itakuwa na wachezaji wengi watakaokimbizana kwenye vitu vya kuwania ufungaji bora kwa kuwa wanaweza kutengeneza ushindi wowote mkubwa kutokana na mabadiliko aliyoyafanya kocha wao.

“Huu ni mwanzo tu kwani tayari kikosi kimesharudi kwenye utimamu wake, hivyo matarajio ya kushinda na kufanya vizuri hasa katika mashindano yaliyo mbele yetu ni makubwa. Mashabiki wetu wakati timu yao inapoteza mechi ilikuwa inawaumiza kuona hawana furaha lakini sasa wamerudisha tabasamu lao,” alisema.

Hivi karibuni Mwanaspoti iliwahi kuripoti kuwa, mabosi wa Yanga wamefanikisha kuwaongezea mikataba nyota wao wawili, Pacome na beki wa kulia Yao Kouassi ambao kila mmoja ataendelea kuvaa jezi za timu hiyo ya Jangwani kwa miaka mingine miwili zaidi.

Pacome ambaye msimu wake wa kwanza tu alifanya makubwa akifunga mabao saba, kiwango chake kiliwavutia mabosi wa Yanga na kuamua kumuongezea mkataba. Kiwango cha staa huyo kilionekana kuwavutia makocha wote wawili kuanzia Miguel Gamondi na Sead Ramovic.