Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Hussein Kazi alivyoweka rekodi Ligi Kuu

Muktasari:

  • Katika msimu huo uliomalizika kwa Yanga kuwa bingwa, Kazi ndiye mchezaji aliyecheza mechi zote 30 bila ya kukosa hata dakika moja akifikisha dakika 2700.

BAADA ya beki wa kati wa Namungo FC,  Hussein Kazi kuweka rekodi ya kuwa mchezaji aliyecheza dakika nyingi za Ligi Kuu ya NBC msimu wa 2025-2026, amezungumzia kitu kikubwa alichojifunza kupitia hilo.

Katika msimu huo uliomalizika kwa Yanga kuwa bingwa, Kazi ndiye mchezaji aliyecheza mechi zote 30 bila ya kukosa hata dakika moja akifikisha dakika 2700.

Beki huyo wa zamani wa Simba, amesema baada ya kuona anategemewa kikosi cha kwanza, alibadili mtindo wake wa maisha kuhakikisha anapokuwa uwanjani huduma yake inakuwa na manufaa kwa timu.

 "Jambo la kwanza nilianza kulala mapema, kutoka kulala saa 6 au saa 7 usiku nilianza kulala saa 3 usiku ili kuupa mwili nguvu, nilikuwa nakunywa maji ya kutosha na kama ikitokea nikachelewa kulala kwa wiki basi ilikuwa mara moja au mbili," amesema na kuongeza;

"Kama unavyojua vijana kuna wakati utapenda kuchati ama kuperuzi mitandaoni hayo pia niliyapunguza sana, badala yake nilitumia muda mwingi kujifua na mazoezi binafsi, kuhusu chakula ni cha kawaida isipokuwa nilizingatia kile cha kuongeza nguvu mwilini."

Alielezea uzoefu aliyoupata kucheza kila mechi dakika 90, alikuwa anapata muda wa kurekebisha makosa na kuwa bora kila mechi.

"Kama binadamu lazima kuchoka lakini  nilihakikisha napumzika vya kutosha ili kuweza kurikava, nilijua timu inanihitaji, hivyo nikajifunza kujilinda na kujitunza, nidhamu ya hali ya juu na kuzingatia maelekezo ya makocha," amesema.

Amesema mechi zote zitasalia kumbukumbu katika msimu uliyoisha, lakini dhidi ya Mtibwa Sugar anaipa umuhimu kutokana na namna ilivyokuwa na presha kubwa.

"Haikuwa mechi rahisi, lakini kikubwa timu imesalia Ligi Kuu, hilo ndilo la msingi," amesema.

Kazi alijiunga na Namungo 2025-2026 akitokea Simba ambako alikuwa hapati nafasi ya kucheza, lakini sasa amefanikiwa kuwa panga pangua kikosi cha kwanza, huku akielezea hilo akisema: "Kitu kinachowafelisha watu wengi siyo tu katika mpira wa miguu, bali hata kazi nyingine ni mtazamo."

Alifafanua: "Kutokupata nafasi Simba nilichukulia kama ni kukosa nafasi napaswa kupambana zaidi, nimepambana na kufanikiwa kuandika rekodi ya aina yake, hicho kwangu ni kitu kikubwa sana.