Huku Mwamnyeto, kule yupo Chama, usipime!

Muktasari:
Taasisi hiyo iliyo chini ya nahodha wa Taifa Stars anayechezea Aston Villa, Mbwana Samata na nyota wa muziki, AliKiba imekuwa ikitumia fedha inazopata katika mechi za aina hiyo zinazochezwa kila mwaka, kutoa msaada kwa jamii.
MASHABIKI wa soka nchini leo wategemee kupata burudani ya aina yake kupitia mechi maalumu ya hisani ya Nifuate2020 iliyoandaliwa na Taasisi ya SamaKiba ambayo itafanyika katika Uwanja wa Taifa leo saa 10.00 jioni, kwani Bakar Mwamnyeto na Clatous Chama wanatarajia kuonyeshana kazi.
Taasisi hiyo iliyo chini ya nahodha wa Taifa Stars anayechezea Aston Villa, Mbwana Samata na nyota wa muziki, AliKiba imekuwa ikitumia fedha inazopata katika mechi za aina hiyo zinazochezwa kila mwaka, kutoa msaada kwa jamii.
Wawili hao wamekuwa wakiunda vikosi viwili vya nyota wa soka kutoka klabu mbalimbali za ndani na nje ya nchi sambamba na baadhi ya watu maarufu na Samatta ametaja skwadi lake likiundwa Juma Kaseja, Shomari Kapombe, Mohamed Hussein, Erasto Nyoni, Kelvin Yondani, Farid Musa, Shaban Chilunda, Iddi Nado, John Bocco na Samatta mwenyewe.
Upande wa AliKiba wapo Bernard Morrison Shaban Kado, Lamine Moro, Bakari Mwamnyeto, Ibrahim Ajibu, Said Ndemla, Abdu Kiba, Mudathir Yahya, Hassan Banda, Tunda Man, David Molinga, Haruna Niyonzima, Said Mussa, Feisal Salum, Meddie Kagere.