Horseed yairudisha Azam Chamazi

Tuesday September 14 2021
azam pic
By Mwandishi Wetu

Mchezo wa marudiano kati ya Azam na Horseed katika kombe la Shirikisho barani Afrika uatakaopigwa Jumamosi Septemba 18 umerudishwa katika uwanja wa Azam Complex badala ya Uhuru.

Akizungumza Ofisa Habari wa  Azam, Thabit Zakaria amesema Horseed wameamua kuamisha mchezo huo kutoka Uhuru hadi Azam Complex baada ya kufurahi miundombinu iliyopo uwanjani hapo

“Horseed wameamua kuamisha mechi yetu Azam Complex baada ya mechi yetu ya awali kupangwa kuchezwa Uhuru na sababu kubwa ni wao kuridhishwa na miundombinu iliyopo Chamazi” anasema Zakaria

Mechi ya kwanza Azam ilishinda mabao 3-1 wakiwa wenyeji wa mechi hiyo.IMEANDIKWA NA LILIAN MUKULU

Advertisement


Advertisement