Hofu ya Morrison wakiifuata Red Arrows Zambia

MSHAMBULIAJI wa Simba, Bernard Morrison alionyesha kiwango bora katika mechi ya mzunguko wa kwanza kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Red Arrows ameonyesha wasiwasi wake akielekea Zambia.
Kikosi cha Simba kiliondoka asubuhi ya leo Desemba 3, 2021 kwenda Zambia kwa ajili ya mchezo wa marudiano ambao utapigwa Desemba 5.
Kupitia kurasa za kijamii, mcheza Bernad Morrison aliweka picha amejifunika na barakoa hadi machoni na kuambatanisha ujumbe ambao ni kama ni ishara ya kujilinda na kubambikiwa Covid-19 huko anakoenda.
“Najaribu kujilinda mwenyewe kabla hawajaenda kusema nina Covid huko Zambia” ameandika Morrison
Katika mchezo wa mzunguko wa kwanza uliopigwa Jumapili katika uwanja wa Benjamini Mkapa, Simba walishinda mabao 3-0, dhidi ya Red Arrows.
Kwenye mchezo huo Morrison alikuwa kwenye kiwango bora kwa alihusika kwenye mabao yote matatu alifunga mawili na kutoa pasi bao kwa Meddie Kagere.