Himid atetema kwa Al Ahly

Thursday June 23 2022
himid pic
By Leonard Musikula

NYOTA wa kimataifa wa Tanzania Himid Mao 'Ninja' anayechezea klabu ya Ghazl Mahalla ya nchini Misri ameendeleza moto wake baada ya kuifungia timu yake bao la kufutia macho dhidi ya Al Ahly walipoambulia kipigo cha mabao 2-1 kwenye mchezo wa Ligi Kuu nchini humo.

Himid aliifungia timu yake bao la kusawazisha mnamo dakika ya 57 ambapo walikuwa nyuma kwa bao moja kisha bao likaresha matumaini ya klabu yake kuondoka na ushindi hadi hapo  Al Ahly walipoumaliza mchezo kwa kufunga bao la pili dakika za mejeruhi na mchezo ukamalizika kwa Al Ahly kuondoka na pointi tatu.

Nyota huyo wa Tanzania amekua akiiongoza safu ya kiungo ya Ghazl Mahalla ambapo hadi hivi tayari amecheza mechi 20 katika 21 msimu huu akiwa na timu hiyo.

Ikumbukwe kuwa Himidi Mao alishawahi kuichezea Azam Fc klaba ya kutimkia nchini Misri na kwenda kuungana na Petrojet, Enppi Sc pamoja Entag El Harby zote zikiwa za nchini Misri. 

Advertisement