Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Hii sasa balaa! Wanawake Arusha, Kilimanjaro wajitokeza kujifunza karate

Muktasari:

Akizungumza katika mafunzo hayo, Joyce Mombuli alisema mchezo huu ni mchezo kama michezo mingine na kuielewa karate lazima uzingatie ujitume na nidhamu.

ARUSHA. JUMLA ya majaji na waamuzi 42 kutoka mikoa ya Arusha na Kilimanjaro wamejitokeza kushiriki mafunzo maalumu ya mchezo wa karate ambayo yameanza kufanyika  katika Ukumbi wa Silk klabu uliopo jijini hapa ambapo wawili ni wanawake.
Akizungumza katika mafunzo hayo, Joyce Mombuli alisema mchezo huu ni mchezo kama michezo mingine na kuielewa karate lazima uzingatie ujitume na nidhamu.
"Mchezo huu si mbaya kama wengi wanavyodhani unakubalika kwa kila MTU Mimi nimekuwa katika karate kwa miaka minne sasa na unanisaidia kujiamini na kuwa na ulinzi mwenyewe nawasihi wanawake wenzangu wajitokeze kushiriki," alisema Mombuli.
Mwenyekiti wa chama cha Karate Mkoa wa Arusha Sensei Dady Kassim ambaye pia ni Mwakilishi wa Shirikisho la Shotokan Karate West Coast Internation (WCSKI), alisema mafunzo hayo ni katika kuwaandaa na kuwaweka sana vijana kwa ajili ya mitihani ijayo mapema mwaka ambapo watafanya mitihani kwa ngazi tofauti tofauti kuanzia Mkanda wa machungwa hadi mweusi yaani digrii ya kwanza.
Akizungumza kushiriki wa wanawake Dady Kassim Alisema kuwa bado uko chini tofauti na nchi za Nigeria, Kenya na Rwanda ambazowanawake wengi wamekuwa wakijifunza karate kuliko wanaume.