Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Hichi ndicho kikosi cha Thank You FC

Muktasari:

  • Azam FC ndio iliyoanza kwa kutangaza kuwatema makocha wake kabla ya kugeukia wachezaji kisha kufuatiwa na Yanga na Simba

LIGI Kuu Bara imemalizika wiki mbili zilizopita na kushuhudiwa Yanga ikitetea taji kabla ya kubeba pia Kombe la ASFC, lakini kwa sasa mashabiki wanapata burudani nyingine kutokana na kuwepo kwa kaligi flani matata ya wachezaji na makocha wanaotemwa na kuagwa na timu kwa 'Thank You'.

Azam FC ndio iliyoanza kwa kutangaza kuwatema makocha wake kabla ya kugeukia wachezaji kisha kufuatiwa na Yanga na Simba, lakini kabla ya thank you za jana, Wanalambalamba walikuwa wakiongoza msimamo wa kugawa 'thank you' nyingi.
Mwanaspoti kupitia thank you hizo zilizotolewa hadi sasa, imetengeneza kikosi kabambe cha wachezaji waliotemwa na makocha hao, sambamba na msimamo wa kaligi hako kalivyo kwa sasa;

Kikosi kilivyo:
Mahmoud Mroivili, Emiry Nimubona, Bruce Kangwa, Joseph Zziwa, Mohamed Ouattara, Victor Akpan, Tuisila Kisinda, Cleophas Mkandala, Rodger Kola, Bernard Morrison na Augustine Okrah

Akiba: Wilbol Maseke, Kenneth Muguna, Dickson Ambundo, Nelson Okwa, Geurold Mwamba wa Mwamba na Djibril Olatunje, Gadiel Michael

Kocha: Fred Felix 'Minziro' na Kally Ongala

Msimamo wa Ligi wa 'Thank You'

1. Simba SC (12)

2. Azam FC (10)

3. Coastal (7)

4.  Namungo (7)

5. Yanga SC (6)

6. KMC FC (1)


7. Geita Gold (1)