Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

He! Hadi Jengua kamaindi bana

Muktasari:

  • Iko hivi. Si unajua kuwa ile kumbukumbu ya staa aliyefanya mapinduzi makubwa kwenye Bongo Movie, Steven Kanumba, ndio inakaribia? Hivyo na itakuwa miaka sita tangu aage dunia.

KUNA ishu inazunguka huko Bongo Movie unaambiwa hadi mkongwe wa filamu, Mohamed Fungafunga ‘Jengua’ ameshutuka na kutema shombo.

Iko hivi. Si unajua kuwa ile kumbukumbu ya staa aliyefanya mapinduzi makubwa kwenye Bongo Movie, Steven Kanumba, ndio inakaribia? Hivyo na itakuwa miaka sita tangu aage dunia.

Sasa wasanii mbalimbali kutoka Kenya waliokuwa wakimzimia Kanumba walitua nchini kurekodi wimbo na video ya Kanumba amerudi, na waliomba ushiriki wa wasanii wa hapa nyumbani pia.

Lakini, walichokutana nacho ndio kimemshtua Jengua na kuamua kuwachamba kinoma baada ya baadhi ya wasanii kutaka walipwe kwanza ndipo washiriki kwenye wimbo huo, ambao baadaye alikabidhiwa mama Kanumba, Flora Mtegoa.

Hata hivyo, kwa mujibu wa kiongozi wa msafara wa Wakenya hao, Paul Leonard ‘Katapila’, walitaka kuwashirikisha wasanii wa hapa nchini, ambao waliwahi kufanya kazi na Kanumba enzi za uhai wake, lakini wote hawakupatikana zaidi ya Jenifer na Patrick watoto waliokuzwa kisanii na staa huyo.

Kitendo hicho sio tu kimewaudhi Wakenya, bali hadi Jengua, ambaye alidai baadhi yao walitaka walipwe hela kwa ajili ya kazi hiyo.

Mama wa Kanumba naye alifunguka, kuna wasanii aliwasailiana nao kwa simu kuhusu ishu hiyo, lakini kwanza wakamuuliza kama kuna hela.

“Nimecheza filamu mbili ama tatu na Kanumba na nilipoambiwa jambo hili sikusita kuja, sasa kwanini wengine waombe hela wakati ni sehemu ya kumkumbuka mwenzetu, ifike mahali wasanii tujitambue,” alisema Jengua.