Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Hanspope, Dk Msolla na Kibadeni watoa neno usajili Simba, Yanga

Muktasari:

“Usajili wa Simba na Yanga kwa kiasi fulani umetikisa, lakini ligi itakapoanza ndipo tutaona kama tunachoaminishwa sasa ndicho kimefanyika katika viwango hasa kwa wageni,”  Kibadeni

Kocha wa zamani wa Simba, Abdallah ‘King’ Kibadeni ameuzungumzia usajili wa timu za Simba na Yanga katika dirisha hili, huku vigogo wa timu hizo, Zacharia Hanspope na Dk Mshindo Msolla wakianika mipango ya klabu zao.

Mpaka sasa Simba imewasajili Bernard Morrison, Lally Bwalya, Chrispin Mugalu, Joash Onyango, Ame Ibrahim, Ilanfya Charles na David Kameta ‘Duchu’.

Kwa upande wake, Yanga imewasajili Sogne Yacouba, Bakari Mwamnyeto, Yassin Mustapha, Zawadi Mauya, Farid Mussa, Kibwana Shomari, Tuisila Kisinda na Mukoko Tonobe.

Kibadeni, nyota wa zamani wa Simba na Taifa Stars amewashauri wachezaji wazawa kutoridhika kuwekwa benchi na wageni, ili wajiuze vizuri katika soko la wachezaji.

“Usajili wa Simba na Yanga kwa kiasi fulani umetikisa, lakini ligi itakapoanza ndipo tutaona kama tunachoaminishwa sasa ndicho kimefanyika katika viwango hasa kwa wageni,” alisema jana katika mahojiano na Mwananchi.

“Lakini kinachonisikitisha ni wachezaji wetu wa nyumbani, tunafahamu sasa mpira ni biashara, wazawa wanapaswa kupambana kila mmoja ajitambue kwani soka ni soko huria, wasiridhike kuwekwa benchi, wajitume.”

Naye mchambuzi wa soka na nyota wa zamani wa Yanga, Ally Mayay alisema mwenendo wa usajili wa Simba na Yanga msimu huu kwa kiasi kikubwa una dalili za kunogesha Ligi Kuu msimu ujao.

“Wachezaji wa kigeni wanaosajiliwa na klabu hizi viwango vyao kwenye ligi wanazotoka vinaonekana, hivyo ujio wao sio tu utaongeza ushindani, lakini pia huenda ukaongeza thamani ya ligi yetu,” alisema Mayay.

Alisema usajili wa wageni unapaswa kuchukuliwa kama changamoto kwa wachezaji wazawa nao kuwa na hamu ya kuona siku moja wanagombaniwa na kuwekewa fedha nyingi mezani za usajili kama ambavyo inafanyika kwa wageni hivi sasa.

Hanspope, Dk Msolla

Akizungumzia kikosi chao, mmoja wa vigogo wa kamati ya usajili ya klabu ya Simba, Hanspope alisema: “Tumefunga usajili, kinachosubiriwa sasa ni shamrashamra kuelekea kwenye Simba Day na kuanza kwa Ligi Kuu.”

Alisema wachezaji wa kigeni tayari wamewapa mkono wa kwaheri akiwamo beki Tairone Santos da Silva, kiungo Sharaf Eldin Ali Shiboub na mshambuliaji wa pembeni, Deo Kanda.

Naye mwenyekiti wa Yanga, Dk Mshindo Msolla alisema katika usajili wa msimu huu wataongeza wageni wapya wanne ambao wataungana na waliopo.

“Hatuna sababu ya kuwa na wachezaji 10 wa kigeni, wakizidi sana tutakuwa nao wanane tu, hivyo kipindi hiki tutaongeza wachache kulingana na uhitaji wa timu na gharama, wageni hawatazidi wanane,” alisema.