Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Haji? Diego huyu hapa

Muktasari:

Baada ya kufichuka, Yanga wakataka kufanya ujio wake uwe siri sana. Wakamshusha Dar es Salaam usiku mnene lakini Kamera za Mwanaspoti ambalo ndio gazeti la Kiswahili linalouzwa zaidi Afrika Mashariki, zikamnasa kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere. Angalia picha zake hapo ukurasa wa mbele.     

MWANASPOTI lilifichua kwa mara ya kwanza usajili wa Mniger, Issofou Boubacar, Jumamosi iliyopita. Simu kibao zikamininika kwenye chumba chetu cha habari, vigogo wa juu wa Yanga wakitaka kujua hiyo ishu imevujaje? Yanga walitaka kufanya siri kubwa na sapraizi ya mwaka kwa mashabiki wao Tanzania nzima.

Lakini Mwanaspoti ilivinyaka vielelezo na kufichua sapraizi hiyo, Yanga wakakosa pumzi kwa vile ilikuwa ni ishu iliyokuwa ikifanywa na watu wachache sana pengine hata na Mwenyekiti Yusuf Manji alisubiri sapraizi hiyo.

Baada ya kufichuka, Yanga wakataka kufanya ujio wake uwe siri sana. Wakamshusha Dar es Salaam usiku mnene lakini Kamera za Mwanaspoti ambalo ndio gazeti la Kiswahili linalouzwa zaidi Afrika Mashariki, zikamnasa kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere. Angalia picha zake hapo ukurasa wa mbele.

Mchezaji huyo ambaye anaelezewa kama mmoja wa viungo wenye akili ya kupanga mashambulizi, alitua Dar es Salaam saa tisa alfajiri ya jana Jumatano, lakini wenyeji wake wakamzuia asizungumze lolote na kumpeleka moja kwa moja Sinza kupumzika.

Kijana huyo aliyecheza zaidi ya misimu mitano nchini Tunisia akipewa jina maarufu la Diego, alianza mazoezi na Yanga jana hiyo hiyo asubuhi kwani alitambulishwa kwa wachezaji wenzake kwenye Uwanja wa Polisi na kufanya mazoezi mepesi kwa dakika chache kisha akaondoka na wakala wake.

Yanga awali ilikuwa ikifanyia mazoezi kwenye Uwanja wa wazi wa Boko Veteran, lakini jana ikahamia Polisi Kurasini ambako ni marufuku Mwandishi wa Habari wala shabiki kuingia.

Diego amekuja kujaribiwa na kama asipomridhisha kocha, Hans Pluijm, atarejeshwa alikotoka na ataletwa mchezaji mwingine kutoka huko huko Afrika Magharibi.

Mara baada ya kutua haikuwa kazi rahisi kwa Boubacar baada ya ya kuzuiwa kwa baadhi ya mizigo na nyaraka zake mbalimbali.

Hali hiyo ilimletea usumbufu kiasi kwani alilazimika kurudishwa ndani ya uwanja wa ndege kutoa maelezo kadhaa yaliyohiyatahija kwa maofisa wa Idara ya Uhamiaji wa uwanjani hapo.