Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

HADITHI: MPANGO ULIOVUJA

Mkuu, nchi nyingi wanaamini uzalendo hupatikana kwenye majeshi ambayo ndiyo mafunzo yao yamejaa uzalendo ushupavu na nidhamu ya hali ya juu. Lakini tumeona wale waliopewa dhamana na nchi ndiyo hao wanaoivuruga nchi. Kwa mfano jeshi la polisi lipo kwa ajili ya kulinda raia na mali  zao lakini kuwa baadhi ya askari si waadilifu wanakula rushwa badala ya kuizuia hata kutumika vibaya kwa ajili ya faida ya mtu mmoja.
“Katika jeshi la  wananchi kuna watu wengine si waaminifu kutokana na kukosa uadilifu wameweka tamaa mbele kwa ajili ya matumbo yao na kuwa tayari kuisaliti nchi hata kufanya mapinduzi au jeshi kuhasi na kuingia porini na matokeo yake inakuwa vita ya nchi na kuuana wenyewe kwa wenyewe.
“Unajiuliza mnawaua ndugu zenu kwa tamaa ya madaraka tu, unajiuliza zile roho za ndugu zako mlizozitoa kwa ajili ya kutaka madaraka zimekosa nini. Unapata nini ukikanyaga damu za ndugu zako ukiingia Ikulu? Najua inauma mpaka sasa kuna watu wangapi kama Gang wapo kwenye nchi za Afrika na wamevaa ngozi ya kondoo na kuonekana watii kwa viongozi wao, lakini mioyoni wana dhamira mbaya.
“Afrika ni bara tajiri sana lakini ni sisi wenyewe ndiyo tunalimaliza kwa tamaa ya matumbo yetu kwa kutumiwa na watu wachache kwa faida yao na matokeo yake umaskini hauishi ni sawa kufa kwa kiu umo ndani ya maji.
“Siku zote mzalendo wa kweli hawezi kuingia madarakani akikanyaga damu za ndugu yake au kuisaliti nchi yake. Si hao tu kuna waliopewa madaraka kuiongoza nchi ukiwa marais mawaziri wakuu na mawaziri wengine waliochaguliwa na mkuu wa nchi kwa ajili ya kumsaidia.
“Hapa napo kuna tatizo kubwa ambalo nalo linaweza kuvunja mioyo wa wananchi na kuwafanya hata wawe tayari kushawishika kuisaliti nchi kwa kuamini ndiyo njia sahihi ya kutatua matatizo yao. Kiongozi akikosa uadilifu unyenyekevu mapenzi ya kweli kwa watu wake majirani zake huwa tatizo kubwa.
“Kiongozi wa juu ukiwa dikteta utaki ushauri unafanya maamuzi kwa faida yako si ya nchi, kiongozi mabadhilifu kiongozi anayejiangalia mwenyewe kisha hatoi haki sawa kwa raia wake  huyohuyo anatangaza amani hapo anajidanganya, sawa na kusema kuna usalama mikono yako imejaa damu.
“Upande mwingine kiongozi wa juu anakuwa safi lakini wasaidizi wake wanamuangusha kwa tamaa zao wanaingia mikataba mibovu kwa ajili ya asilimia kumi. Wengine wanajilimbikizia mali huku mamilioni ya wananchi wake hawana maji, afya bora elimu. Ukiona mtu wa aina hii hana uzalendo na si wale wa nchi yangu kwanza.  
“Mkuu, Vitu vyote hivi dawa yake ni uzalendo wa kweli, uongozi uliotukuka kuwatumikia waliokuchagua kusikiliza ushauri wenye tija kutoa haki sawa kwa wote kuchukia ubadhilifu rushwa uzembe toka chini ya uvungu wa moyo wako. Ukiyafanya haya na somo la uzalendo la nchi yangu kwanza hakika hakuna mamruki atakayeingia ndani ya nchi.
“Uzalendo wa kweli unapatikana kwa kupikwa na si kuchemsha. Inatakiwa  elimu ya uzalendo ifundishwe kuanzia shule za msingi kama kuuimba wimbo wa taifa. Mtoto  ajifunze kuijua nchi yake ajijue yeye ni nani na kwa nini yupo pale nini zipi rasilimali za nchi nani mwenye  jukumu ya kuilinda. 
“Pili amani ya nchi yake inatokana na nini na nini kunaondoa amani kipi akikifanya atakuwa ameisaliti nchi yake. Vitu hivi vichache vikifundisha toka elimu ya msingi mpaka chuo kikuu kwa nini mtu asiwe mzalendo na kusema nchi yangu kwanza.
“Kama mtu anaweza kusoma kuanzia elimu ya sekondari mpaka chuo kikuu anakuwa daktari bingwa. Kwa nini mtu asiwe mzalendo wa kweli? Mzalendo wa kweli hawezi kuisaliti nchi yake siku zote nchi yake huwa kwanza kisha kitu kingine kinafuata. Mzalendo wa kweli hawezi kula rushwa, mzalendo wa kweli hawezi kutega kazi mzalendo wa kweli hawezi kuharibu miundo mbinu.
“Hivi vyote vikisimamiwa na utawala bora hebu niambie Gang angepata wapi uthubutu wa kuisaliti nchi yake? Angekuwa tayari kufa na si kuisaliti nchi yake au kuona damu ya watu wasio na hatia inapotea bure.”
“Uhuuu!” mkuu wa nchi alishusha pumzi ndefu baada ya kusikia madini adimu toka kwa binti mrembo.Ilikuwa kama ndiyo siku ya kwanza kuingia darasa la uzalendo na mwalimu wake binti mrembo sawa na mwanaye wa mwisho. Malik alijikuta akichekelea moyoni huku akiamini darasa na Kanali Hassani limefanya kazi. Mkuu wa nchi baada ya kushusha pumzi ndefu aliwageukia wakuu wake wa jeshi na waziri wa ulinzi na kumtazama kila mmoja kisha alisema:
“Yote yaliyosemwa mmeyasikia?” aliwauliza kwa sauti kubwa.
“Ndiyo mkuu,” waliitikia kwa pamoja kwa sauti ya ukakamavu.
“Binti mdogo lakini ameshiba uzalendo, katika dunia ya leo binti mrembo kama huyu amejitoa muhanga kwa ajili ya Afrika yake lakini ninyi mnaopewa kila kitu ndiyo wasaliti namba moja. Nataka yote yaliyosemwa yafanyiwe kazi mara moja na hili nitalifuatilia hatua kwa hatua.
“Kuanzia mwakani elimu ya uzalendo itaanza tokea darasa la kwanza mpaka chuo kikuu na maksi zake ndio zitamfanya mtu kuingia sekondari mpaka chuo kikuu pia kila atakayesomea uzalendo atapata mkopo wa bure watu hao watapewa kipa umbele katika nchi yetu hata kama sipo madarakani.”
“Sawa mkuu.”
“Mkuu nilikuwa na ombi,” Malik alitoa ombi.
“Sema kijana wangu.”
“Hawa ndugu zangu naomba wapewe zawadi na kupandishwa vyeo ni watu ambao wamenionesha wanaipenda nchi yao kwa dhati.”
“Hakuna shida kila kitu kitakwenda kama ulivyoomba,” mkuu wa nchi alikubali.
“Malik,” mkuu alimwita Malik.
“Naam mkuu.”
“Nina imani kuna sababu zilikuleta hapa tofauti na hili lilivyotokea hasa kutokana na mazungumzo yako na Gang.”
“Ni kweli.”
Malik alimweleza kilichompeleka pale mpaka hatua ile kuwa pale, simulizi ile ilikuwa kama filamu ya kijasusi iliyokuwa ikisisimu. Kila mmoja aliyekuwa mule ndani aliwatazama Malik na Queen akiwa haamini kilichokuwa kikisemwa.
“Ooh! Poleni sana.”
“Tupe hongera mkuu.”
“Hongereni.”
“Asante.”
“Najua bado mna safari ndefu, naomba mseme mnataka nini kwangu ili tu kuhakikisha mnafanikiwa katika kampeni yenu nzito ambayo inanitetemesha moyo wangu.”
“Mkuu msaada mkubwa kwako ni usafiri wa kwenda Ujerumani na kurudi Tanzania tu.”
“Huo mmepata kingine?”
“Silaha za kisasa.”
“Mmepata, kingine?”
“Kwa leo ni hayo tu mkuu.”
“Mnataka kuondoka lini?”
“Hata sasa hivi kama kuna usafiri.”
“Mkuu na mimi nilikuwa naombi?” John mpelelezi wa Sudani ya Kusini alitoa ombi.
“Ombi gani?”
“Kwa vile kaka Malik na dada Queen wamejitoa kwa ajili ya nchi yetu nami naomba niungane nao katika safari yao ya Ujerumani kutokana na maelezo yako nina imani ninahitajika katika mambo ya IT kwa ajili ya Afrika yangu.”
Malik kabla ya kujibu alimtazama Queen ambaye hakuonesha chembe ya wasi kwa John.
“Sawa,” alikubali.
“Na mimi,” Sonia mpelelezi wa kike naye alitaka kuungana na kina Malik.
Malik kutokana na kuufahamu uwezo wake hakupinga naye alimkubalia.
“Nashukuru,” Sonia alishukuru kukubaliwa kuungana na kina Malik.
“ Kunche chukua ndege ya kukodi hadi Sudani kisha wapande ndege kubwa hadi wanapokwenda, hakikisheni zinapatikana tiketi nne kwenda na kurudi. Mbili Sudani Ujerumani Tanzania na mbili Sudani Ujerumani Sudani, ” mkuu alitioa amri.
“Sawa mkuu.”
“Sasa vijana wangu si mpumzike ili muondoke jioni, najua mmechoka sana,” mkuu wa nchi alitoa wazo.
“Mkuu siku zote jambo langu kama halijakamilika siwezi kuchoka, nitapumzika pale nitakapo maliza kilichonitoa nyumbani au nikifa,” Malik alijibu.
“Mnataka muondoke saa ngapi?”
“Kama usafiri upo hata sasa hivi.”
“Nimekuelewa inaonesha jinsi gani uzalendo umejaa moyoni mwako.”
“Naipenda sana nchi yangu naipenda sana Afrika yangu napenda sawa haki,  usawa na upendo vyote hivyo uleta amani.”
“Sawa kijana wangu mtakwenda kupumzika mkisubiri safari yenu nimepata taarifa ndege ya Emirates itatua Uwanja wa ndege wa kimaitafa wa Khartoum Sudan saa tatu asubuhi na kuondoka saa tano.”
“Sawa mkuu.”
Malik na wenzake walipelekwa sehemu kwa ajili ya kupumzika kwa muda wakati huo ilikuwa saa nane za usiku. Ilikuwa tofauti na walivyofikiria kuwa Malik na Queen wangelala lakini baada ya kuingia chumbani muda mwingi walitumia katika mikakati mizito juu ya safari yao.
Kuongezeka kwa John kuliwaongezea kujiamini hasa kutokana na uwezo wake wa kucheza na vitu vya IT. Kingine kilichoongeza hamasa kilikuwa jinsi John na Sonia walivyokuwa na furaha ya kufanya kazi nao. Ilikuwa tofauti mtu akisikia safari ya kifo alikaa nyuma mpaka alazimishwe lakini kwao ilikuwa tofauti hawakuwa na chembe ya wasi.
                                                                         MAKAO MKUU.
Mkuu wa usalama wa taifa alikuwa bado yupo ofisini kwake akiendelea kuhakikisha kila kitu kinakwenda salama. Siku zote kukiwa na kazi nzito Chifu Juma Shila  alikuwa halali alikuwa na uwezo wa kukesha siku tatu bila kulala na wala usijue. Baada ya kuhakikisha kila kitu kimekwenda vizuri kwa Malik, alisubiri taarifa ya vijana wake aliowatuma kuchunguza mwenendo wa marehemu Manon.
Baada ya muda vijana waliwasiri  na taarifa  ambayo walimpatia bosi wao ambaye aliipitia iliyoonesha vitu vyote vilivyotajwa vinamilikiwa na taasisi ya Asante Afrika (AA) vipo chini ya jina la mtu wa ndani ya nchi na si Manon kama ilivyokuwa ikijulikana.
 Taarifa ile ilishtua  kukuta jina la Medady Mpapai ndiye mmiliki mkuu na wale wengine walikuwa wafadhili tu. Baada ya kusoma mara mbili aliwageukia vijana wake na kusema:
“Mmegundua nini?”
“Mchezo ni uleule wa kumuingiza mtu chaka kisha wanafanya yao mkishtuka mnakuta wao hawahusiki.” Hans alisema.
“Kama Mpapai alikuwa mtu muhimu kwa nini wamemuua?” Moland aliuliza.
“Hakuwa na muhimu kwani vitu walivyovitaka  wamevipata kama angendelea kuishi angeweza kuwaharibia siku moja.” Ngumije alimjibu Nyemo huku Chifu akiwasikiliza.
“Mmh! Kweli wajinga ndiyo tuliwao hawa watu wametutumia wanavyotaka,” Nyemo alisema.
“Wamekuwa kama wawindani wanakuwekea mnofu ukitaka kuufaidi wanakumaliza,” Ngumije alisema.
“Afrika bado tunakazi nzito,” Hans alisema.
“Taarifa ya Sudani Kusini mmeisikia?” Chifu aliwauliza.
“Hapana kuna nini?” wote waliuliza kwa pamoja.
Aliwaelezea kilichotokea Sudani ya Kusini na safari ya Malik na Queen ya kuelekea Ujerumani.
“Mkuu, kwa nini Malik ametuacha?” aliuliza Nyemo.
“Mkiona hivyo mjue kuna kitu amekiona hivyo kinatakiwa kufanyika kwa haraka.,” Chifu alijibu.
“Kile kichwa kuna kipindi sijui jamaa ana ubongo wa aina gani siku zote anachokiwaza lazima kikuache mdomo wazi,” Moland alisema.