Gor Mahia yataka kumrudisha Onyango Kenya

KLABU ya Gor Mahia ya nchini Kenya imeanza mazungumzo na beki wa Simba, Joash Onyango kwa ajili ya msimu ujao.

Beki huyo raia wa Kenya licha ya kucheza mara kwa mara ndani ya kikosi hicho, huenda akarejea kwao baada ya msimu huu kuisha kutokana na kile kinachoonekana kutokubalika na mashabiki wengi.

Mwanaspoti linatambua licha ya Gor Mahia kumhitaji, Singida Big Stars nayo inahitaji saini yake.