Gomes noma sana

Saturday February 20 2021
New Content Item (2)
By Thobias Sebastian
By Clezencia Tryphone

KOCHA wa Simba, Mfaransa Didier Gomes akilala akiamka ni yeye na Al Ahly tu na amesisitiza kwamba lazima wawap-indue kwenye Uwanja wa Mkapa Jumanne bila kujali kwamba ni mabingwa watetezi wa michuano hiyo ya Afrika.

“Nimeangalia mechi zao nyingi na kubaini ambavyo wanacheza katika kusham-bulia wapo bora kwenye maeneo gani na wakishambuliwa wanakuwa na mapungufu wapi na hayo yote tutayachukua ili kuwazuia na kuwashambulia,” alisema.

“Baada ya kuwaangalia na kuyaona hayo yote tulifanya vikao mbalimbali na wasaidizi wangu pamoja na wachezaji wote waliokuwepo ndani ya timu na kuwaonyesha kimoja baada ya kingine am-bacho tuna-hitajika kukifanya katika mechi hiyo,” alisema.

“Mapokeo ya wache-zaji ni makubwa na katika muda huu uliobaki tunakwenda kuyafanyia kazi katika kiwanja cha mazoezi ili kuona ambavyo tutakwenda kuyafanyia siku ya mechi kwa ukamilifu na kuwazidi Al Ahly.

“Hili la kuangalia mechi mbalimbali za Al Ahly kupitia lininga linafanyiwa kazi na mtaalamu wetu husika, Culvin Mavunga ambaye tumekuwa tukisaidiana kuwapatia wachezaji wetu na tumefanya hili hata katika mechi na AS Vita mpaka kufanikiwa kupata pointi tatu,” alisema Gomes.

“Siku moja kabla ya kucheza mechi na AS Vita nilifanya kikoa na wachezaji wangu ambao niliwapatia tena video mbalimbali za wapinzani wetu na kuwakum-busha yale yote ambayo tunayahitaji na tuliyafanyia kazi katika mazoezi,” aliongezea.

Advertisement

Katika hatua nyingine Gomes alisema amelizika na viwango ambavyo vimeonyesha na wachezaji wake licha ya ratiba kuwataka kucheza mechi nyingi ndani ya siku chache lakini hata mazingira ya kiwanja yalikuwa si mazuri.

“Wachezaji wangu ambavyo wanajituma naimani kubwa tukiwa na muendelezo huu tutafanya vizuri zaidi na kutetea ubingwa wa ligi ambao utatupa nafasi ya kucheza Ligi ya mabingwa Afrika msimu ujao,” alisema.

“Tunaendelea kuyafanyia kazi yale mapungufu yetu ambayo tumeyaonyesha katika mchezo uliopita ili kuimarika na kufanya vizuri katika mechi zinazofuata na ubora wa wachezaji wangu ulivyo hilo linawezekana,” alisema Gomes.


TSHABALALA NAE

Nahodha msaidizi wa Simba, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ alisema wamepata matokeo mazuri mfululizo katika mashindano yote kutokana na maandalizi mazuri ambayo wamekuwa wakiyafanya.

“Tumeanza mashindano haya kwa kufanya vizuri mechi ya ugenini nia yetu ni kuwa na muendelezo wa kushinda ili kukusanya pointi nyingi ambazo zitatuweka katika mazingira mazuri kwenye kundi,” alisema.

“Nafasi ya Simba katika Ligi ya mabingwa Afrika mpaka wakati huu tupo katika muelekeo mzuri kwani kupata ushindi katika mashindano haya ukiwa ugenini si kazi rahisi, ila mwenendo wetu katika ligi nao ni mzuri na tutajitahidi kushinda mfululizo ili kufikia malengo yetu ya kutwaa ubingwa,” alisema.

“Morali ya wachezaji imeongezeka na ninakubwa sana hilo limechangiwa baada ya kushinda mechi yetu ya ugenini dhidi ya Biashara United na naimani tutapambana kadri ambavyo tutaweza ili kuona pointi tatu zinabaki kwetu.

“Wachezaji wenzangu zikibaki siku chache kama hizi kabla ya kucheza mechi kubwa na ngumu ya aina hii tunakuwa bize na kufikiria zaidi wapinzani kuliko kufanya jambo lingine lolote lakini tunaomba mashabiki wetu wajitokeze kwa wingi kwani tunatambua mchango wao na tunawahidi tutapata ushindi,” alisema Tshabalala ambaye ni miongoni mwa wachezaji wanaoaminika sana na mashabiki kutokana na moyo wake wa kupambana uwanjani.

Advertisement