Ghalib: Twendeni tukaipe nguvu Stars

Wakati masaa yakizidi kukatika kuekekea muda wa mchezo kati ya Taifa Stars dhidi ya DR Congo Mwenyekiti wa Kamati ya Ushindi ya Taifa Stars Ghalib Said Mohamed 'GSM' amewataka Watanzania kujitokeza kwa wingi uwanjani.

Katika ujumbe wake ambao ameutoa saa chache zilizopita GSM amesema endapo Stars itafanya kweli na kushinda mechi hiyo dhidi ya Congo na ule wa Novemba 14 dhidi ya Madagascar utaipa Tanzania nafasi kuongoza kundi J na hatimaye kuingia hatua ya mwisho ya nchi 10 bora.

"Hatua hii ya kumi bora itatoa nafasi ya timu tano zitakazo wakilisha bara letu la Afrika katika Fainali za Kombe la Dunia nchini Qatar mwakani,imesema taraifa hiyo kutoka kwa GSM.

"Natoa wito kwa Watanzania wenzangu kuiombea timu yetu ya taifa na pia kujitokeza kwa wingi  kushangilia katika michezo hii miwili itakayoenda kujenga historia mpya katika taifa letu."

Stars aqmbao ndio vinara wa Kundi J wakiwa na pointi 17 wanahitaji ushindi kuweka hai kuvuka hatua hii ya makundi ambapo baaa ya mchezo wa leo itasafiri kuelekea nchini Madagascar katika mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi.