Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Fifa kumrejesha Malinzi TFF

Jamal malinzi

MWANDISHI WETU UJUMBE wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa), unaweza kuwarejesha wagombea wa nafasi zote walioenguliwa na Kamati ya Rufaa ya Uchaguzi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF). Katika kikao cha TFF na Wizara ya Michezo kilichofanyika Jumanne wiki hii walikubaliana kuendelea na mchakato wa uchaguzi, lakini kwa masharti kwamba: "Uchaguzi uwe huru na haki, na haki hiyo ionekane kutendeka." Ili haki ionekane kutendeka, hapana shaka wagombea walioenguliwa na Kamati ya Rufaa ya TFF watarejeshwa. Uchunguzi wa Mwanaspoti unaonyesha kuwa wagombea walioenguliwa katika Kamati ya Rufaa, wana nafasi kubwa ya kurejeshwa na ujumbe wa Fifa ambao utakuja hivi karibuni kusikiliza malalamiko yao ya kuenguliwa. Miongoni mwa wajumbe wenye uhakika wa kurejeshwa ni mgombea urais wa TFF, Jamal Malinzi, ambaye kamati ya rufani ilisema hana uzoefu wa miaka mitano. Hata hivyo, Malinzi ametuma wasifu wake kwa Mwanaspoti na kuonyesha kuwa ana uzoefu wa muda mrefu katika masuala ya michezo. Katika nyadhifa mbalimbali alizoshika, inaonyesha kuwa Malinzi ana uzoefu wa miaka 14 katika uongozi wa michezo ingawa baadhi ya wakati alikuwa akiongoza nafasi zaidi ya mbili kwa wakati moja. Malinzi alikuwa Mjumbe wa Baraza la Ushauri Yanga kuanzia mwaka 1999 mpaka 2001 kabla ya kuwa Mkurugenzi wa kuchaguliwa katika klabu hiyo 2001-2002. Alikuwa Kaimu Katibu Mkuu Yanga mwaka 2002-2003, kabla ya kuwa Katibu Mkuu wa klabu hiyo 2003-2005. Alikuwa Mwenyekiti wa Kamati ya mashindano ya Chama cha Soka Mkoa wa Pwani (Corefa) mwaka 2008 mpaka 2010 kabla ya kuwa Mjumbe wa Baraza la Michezo Mkoa wa Dar es Salaam mwaka 2009 mpaka 2012 na Mjumbe Mkutano Mkuu Mkoa wa Kagera 2012-2013 kabla ya kuwa Mwenyekiti Mkoa wa Kagera mwaka 2012 mpaka sasa. Katika sehemu mbalimbali ambako wajumbe wa Fifa wamekwenda kusuluhisha migogoro ya uchaguzi wamekuwa wakiwarejesha wagombea wote ili wapigiwe kura na wajumbe. Mwaka 2004, Fifa kupitia mjumbe wake Joseph Mifsud ilimrudisha katika uchaguzi, Crescentius Magori na watu wengine waliokuwa wameenguliwa na Kamati ya Uchaguzi iliyokuwa inaongozwa na Llyod Nchunga. Baada ya kurejeshwa, Magori alishinda uchaguzi na kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa TFF, lakini hakugombea tena nafasi hiyo katika uchaguzi uliofuata mwaka 2008 kwa madai ya kuwa na majukumu mengi kazini kwake NSSF.