Fei Toto, Morris waipa mzuka Zanzibar Heroes

Muktasari:
Wachezaji ambao wanajumuisha kikosi hicho kwa hatua ya awali upande wa walinda mlango ni Abdul-latif Said Masoud (Jamhuri), Mohamed Abrahman (JKT TZ), Mohamed Muali (Polisi TZ), Abdallah Rashid ‘Babu’ (Ruvu Shooting), Haji Juma ‘Chafu’ (JKU) na Ahmed Ali ‘Salula’ (Malindi).
TIMU ya soka ya taifa ya Zanzibar ‘Zanzibar Heroes’, imeanza mazoezi rasmi juzi katika uwanja wa Amaan mjini Unguja chini ya kocha mkuu Hemed Suleiman ‘Moroko’.
Mazoezi hayo ni moja ya hatua ya kusaka timu ndogo kutoka kati ya wachezaji 40, waliotwa awali, lakini pia ni sehemu ya kujiandaa na mashindano ya Chalenj ambayo yanatarajiwa kuanza Desemba Mosi hadi 19, mwaka huu nchini Uganda.
Wachezaji ambao wameanza mazoezi ni wale ambao wanacheza ligi ya Zanzibar pekee, wakati wale wanaocheza ligi za Tanzania Bara watajiunga na timu siku za mbele.
Wachezaji ambao wanajumuisha kikosi hicho kwa hatua ya awali upande wa walinda mlango ni Abdul-latif Said Masoud (Jamhuri), Mohamed Abrahman (JKT TZ), Mohamed Muali (Polisi TZ), Abdallah Rashid ‘Babu’ (Ruvu Shooting), Haji Juma ‘Chafu’ (JKU) na Ahmed Ali ‘Salula’ (Malindi).
Mabeki ni Suleiman Said Juma (Zimamoto), Mohammed Othman Mmanga (Polisi TZ), Ibrahim Mohamed ‘Sangula’ (KVZ), Mwinyi Haji Ngwali (KMKM), Juma Kukuti Adam (Polisi Tz) na Ally Haji (Mwenge).
Wengine ni Abdul Malik Adam (Mafunzo), Ali Juma Maarifa (Malindi), Issa Haidar Dau (JKU), Abdallah Kheir (Azam), Ibrahim Ame Mohammed (Coastal Union), Ally Ally (Yanga), Abubakar Ali (Mlandege), Ibrahim Hamad (Malindi), Agrey Morris (Azam) na Abubakar Ame ‘Luiz’ (Malindi). Viungo ni Abdul aziz Makame (Yanga), Abdul Swamad Kassim (Kagera), Awesu Awesu (Kagera), Mudathir Yahya (Azam), Ishaka Said (KMKM), Adam Ibrahim ‘Edo’ (KMKM), Kassim Suleiman (Azam), Haroun Abdallah (Zimamoto), Feisal Salum (Yanga), Mohamed Issa (Yanga), Mustafa Muhsin ‘Park’ (Zimamoto) na Helefin Salum (Mlandege). Wengine ni Baraka Shaaban (Ruvu Shooting), Khalid Shaaban (Rich boys), Abdallah Hassan Nassor ‘Abal’ (Polisi TZ), Mohammed Mussa (Mbeya City), Mohamed Abdallah (Mlandege), Ally Juma ‘Larson’ (Mafunzo)
Washambuliaji ni Ibrahim Hamad ‘Hilika’ (Zimamoto), Abdul nassir Asaa (Mlandege), Khamis Mussa ‘Rais’ (Malindi), Said Salum ‘Eto’o’ (Kipanga), Ibrahim Abdallah ‘Imu Mkoko’ (Malindi) na Mussa Ali Mbarouk (KMKM).
Kwa sasa, timu hiyo ya Zanzibar imeanza mazoezi ya awali ikitarajiwa yatachanganya kadri muda unavyoenda.