Fei Toto hatihati kuivaa Polisi Tanzania kesho

Arusha. Kiungo wa Yanga, Feisal Salum 'Feitoto' huenda akaukosa mchezo wa ligi kuu Bara dhidi ya Polisi Tanzania itakayopigwa kesho Jumapili katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha baada ya afya yake kutokuwa imara.
Feisal ni miongoni mwa wachezaji wa Yanga ambao nyota yao imewaka msimu huu kwani katika alama 32 ambazo timu hiyo imekusanya kwenye michezo 12 ilizocheza amehusika moja kwa moja ambapo pia amefunga mabao manne kati ya 22 ambazo Wananchi wamefunga mpaka sasa kwenye ligi ,akiwa pia ni mfungaji namba mbili w timu nyuma ya Fiston Mayele mwenye mabao sita.
Kocha wa Yanga, Mohamed Nabi amesema mchezaji huyo huenda asicheze kutokana na majeraha madogo ambayo yanamkabili lakini uhakika atapata katika mazoezi ya leo kama atakuwa fiti au ataanzia katika benchi na kuongeza kuwa hana wasiwsai kwani Yanga ni timu kubwa na wachezaji wote ni wazuri.
Ameongeza kuwa mchezaji mwingine ambaye anaweza kukosena katika mchezo wa kesho ni kiungo Mukoko Tonombe ambaye amejiunga na timu lakini hajui kama yuko fiti huku winga Chico Ushindi ambaye amesajiliwa dirisha dogo akitokea Tp Mazembe ya Congo DR yeye atapata nafasi ya kucheza dakika chache.
“Tuko vizuri maandalizi yamekamilika kikosi kiko katika hali nzuri tmefanya mazoezi ya kutosha hivyo naamini tutashinda”alisema Nabi.
Nabi ameweka wazi kwamba anatambua anaenda kukutana na timu nzuri ambayo nayo imejipanga kutaka kushinda lakini ni mchezo muhimu kwa upande wao kushinda hili kuendelea kuwa juu kwenye msimamo na kutengeneza njia rahisi ya kutwaa ubingwa ambayo ndio malengo yao.
Kwa upande wake kocha msaidizi wa Polisi Tanzania, Geogre Mketo amesema wanatambua wanakwenda kucheza na timu ambayo inaongoza ligi hivyo wataingia uwanjani kwa kuwaheshimu lakini pia kwa kupambana kubakisha alama tatu muhimu nyumbani.
Amesema wao wala hawana shida na uwanja kwani Ushirika ni sawa na Sheikh Amri Abeid hivyo mashabiki wao wajitokeze kwa wingi kuja kuishangilia timu huku wakishuudia burudani safi kutoka kwa maafande hao.
Naodha wa Polisi Tanzania FC, Juma Ramadhan Haji ametumia fursa hiyo kuwaomba radhi mashabiki wa soka Mkoa wa Kilimanjaro ambao walikuwa na matumaini kwamba mechi itapigwa katika uwanja wa Ushirika huku akiwahidi ushindi keso.
Yanga ndio vinara wa ligi kuu Nbc kwa alama 32,wameshinda michezo kumi na sare mbili,wakati amabapo imefunga mabao 22 na kufungwa nne huku Polisi Tanzania ikiwa na alama 18,imeshinda nne sare sita na kupoteza miwili,ikiwa imefunga mabao 11 na kufungwa nane ,utofauti wa alama ikiwa ni 14 baada ya timu hizo kucheza mechi 12.