Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Fei afungukia bao lake kwa Yanga

Muktasari:

  • Yanga imekubali kichapo cha mabao 2-1 dhidi ya Azam, ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Bara raundi ya 20 uliopigwa kwenye Uwanja wa Mkapa.

Kiungo wa Azam Feisal Salum, Fei Toto, amesema pamoja na kwamba amefanikiwa kuifunga Yanga, lakini timu hiyo ni bora kwenye Ligi Kuu Bara.

Yanga imekubali kichapo cha mabao 2-1 dhidi ya Azam, ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Bara raundi ya 20 uliopigwa kwenye Uwanja wa Mkapa.

Yanga ilianza kujipatia bao kupitia kwa Clement Mzize, lakini Azam wakajibu mapigo kwa mabao ya Jibril Sillah na Fei Toto na kuifanya timu hizo ziendeleze moto wa kuwania ubingwa wa ligi msimu huu.

Fei amefanikiwa kufunga bao lake la kwanza dhidi ya waajiri wake wa zamani likiwa ndiyo la ushindi kwa timu yake ambayo sasa imesogea nafasi ya pili ikiwa na pointi 48, nne nyuma ya Yanga iliyopo kileleni.

Akizungumza na Mwananchi baada ya mchezo huo, Fei alisema bado Yanga ni timu bora kwenye ligi na anaamini inaweza kufanya mambo makubwa.

"Tumeifunga kweli Yanga lakini nataka kukuhakikishia kuwa hii ni timu bora ina wachezaji wazuri.

"Hata kama tumepata ushindi, lakini haimaanishi kuwa wenyewe ni wabovu, hapana, huu ni mpira lolote linaweza kutokea ndani ya dakika tisini tumecheza vizuri ndiyo maana tumeshinda," alisema Fei baada ya mchezo kumalizika.