Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ethiopia inasogea mbele Taifa Stars inatazama tu

Kikosi cha Ethiopia

Muktasari:

  • Tofauti na Tanzania, mashabiki wengi wanaovaa jezi ni wale ambao wana mpango wa moja kwa moja kwenda uwanjani. Wasiokuwa na mpango wa kwenda uwanjani, wanavaa jezi za Manchester United, Arsenal, Liverpool, Chelsea na kwenda vibandani kuangalia mechi za Ulaya huku wakiulizia kinachoendelea Uwanja wa Taifa.

WAKATI timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars ikipiga hatua saba mbele kisha kumi nyuma na kujipongeza, Ethiopia inaonekana kusonga mbele bila ya kurudi nyuma licha ya kuchapwa 2-1 nyumbani katika pambano la kwanza la kufuzu kwenda Kombe la Dunia (Play off) dhidi ya Nigeria.

Nilikuwepo Addis Ababa Jumapili iliyopita kutazama pambano lao dhidi ya Nigeria na ni wazi kwamba Ethiopia haipo tena katika anga za Tanzania. Ushabiki wao katika soka unaipeleka mbali timu yao.

Jezi vazi la taifa

Ethiopia ina idadi ya watu wanaokadiriwa kufikia 80 milioni. Jiji la Addis Ababa peke yake linakadiriwa kufikia idadi ya watu milioni tano. Na katika siku ya pambano la Nigeria, karibu nusu ya wakati wa jiji la Addis Ababa, hasa eneo la katikati ya mji walikuwa wamevaa jezi za timu yao ya taifa.

Achilia mbali jezi, wengine walikuwa wamevaa skafu huku biashara kubwa zaidi katika jiji hilo ikiwa ni kupakaa rangi za bendera ya Ethiopia katika sura za mashabiki.

Kilichovutia zaidi ni ukweli kwamba, wakati dunia nzima ikiamini kuwa wanawake wa Ethiopia ni warembo, wanawake wenyewe wamepeleka mapenzi yao makubwa katika soka kiasi cha kuutia morali mchezo wenyewe. Mabinti wengi walionekana wametinga jezi wakizurura mitaani kusaka tiketi.

Majaliwa Mbasa, mmoja kati ya wadau wakubwa wa soka nchini ambao mara kwa mara husafiri kwenda nje ya nchi kutazama soka la kimataifa, muda mwingi alionekana kupiga hesabu ya mauzo ya jezi.

“Jezi moja ni Birr 350 ambazo ni sawa dola 18, sasa kama nusu ya wakazi wa Jiji la Addis Ababa wamevaa jezi unafikiri watakuwa wameingiza kiasi gani? Ni mamilioni ya pesa,” anasema Mbasa.

Mashabiki nje, ndani

Uwanja wa Addis Ababa unachukua mashabiki 35,000 tu. Lakini kama nusu ya wakazi wa jiji hilo walivaa jezi za Ethiopia, ina maana wengi walikubali kulifuatilia pambano hilo nje ya uwanja, kuliko idadi ya mashabiki ambao walilifuatilia pambano hilo ndani ya uwanja.

Tofauti na Tanzania, mashabiki wengi wanaovaa jezi ni wale ambao wana mpango wa moja kwa moja kwenda uwanjani. Wasiokuwa na mpango wa kwenda uwanjani, wanavaa jezi za Manchester United, Arsenal, Liverpool, Chelsea na kwenda vibandani kuangalia mechi za Ulaya huku wakiulizia kinachoendelea Uwanja wa Taifa.

Kutokana na uwanja wao kuchukua idadi ndogo ya mashabiki, watu wengi walilazimika kulipa viingilio kuingia katika ukumbi mpya wa kisasa wa Millenium unaojaza mashabiki zaidi ya 5,000 kwa ajili ya kutazama mechi hiyo kwa pamoja.

Wengine walijibanza katika kila baa kutazama mechi hiyo, wengi wakiwa na uhakika mkubwa kwamba Ethiopia ingeshinda pambano hilo.

Ethiopia kocha mmoja, Tanzania milioni 45

Taifa Stars ikichapwa, kila shabiki anageuka kuwa kocha mtaalamu kuliko Sir Alex Ferguson au Arsene Wenger. Utasikia tu “Pale angecheza Chuji halafu Kazimoto angesogea mbele, Kiemba akaingia kati, huyu kocha hajui kitu anachukua pesa zetu tu.”Lakini baada ya Emmanuel Emenike kuipiga Ethiopia mabao mawili, kila shabiki alishika njia yake na kuanza kurudi nyumbani. Hakukuwa na makundi makundi ya mashabiki kama yale ya Uwanja wa Taifa ambayo huibuka baada ya mechi na kisha kila mtu anajigeuza kuwa Ferguson.

Nilipowauliza kuhusu kipigo cha timu yao, wao walisema wanamuachia kocha afanye kazi yake kwa sababu anajua kilichotokea zaidi yao, wengine walisema kwamba wachezaji wao walikuwa wachanga dhidi ya mastaa wa Nigeria.

Haishangazi kuona Ethiopia inasonga mbele. Miaka kadhaa iliyopita walikuwa wanaleta vijana katika Uwanja wa Taifa kwa ajili ya kushiriki michuano ya mikubwa kama ya Cecafa. Kwa tabia ya uvumilivu ya mashabiki wao kuondoka uwanjani bila ya kujifanya makocha, ndio maana sasa wanavuna matunda.

Marcio Maximo alikuja na msingi wa soka la vijana na nidhamu, lakini miaka michache baadaye, kila mtu akajigeuza kocha. Kama angewapata mashabiki kama wa Ethiopia, si ajabu sasa tungekuwa mbali.

Bekele ni zaidi ya Obi Mikel

Kiungo mwenye umbo dogo wa Ethiopia, Shemelis Bekele ambaye ni kipenzi cha mashabiki wengi wa Tanzania waliokuwa wanamuona akiwa amevaa jezi namba 7 katika Uwanja wa Taifa, pia ni kipenzi cha mashabiki wa Ethiopia.

Ingawa si kweli, lakini Waethiopia wanaishi kwa imani. Wanaunda kitu ambacho wenyewe wanakubaliana na kukiamini kama ambavyo walijiaminisha kuwa Bekele ni bora kuliko kiungo wa Chelsea, Obi MIkel.

Lengo lao ni kuwatia moyo wachezaji wao na kuiweka Nigeria katika mazingira magumu ya mchezaji. Popote ambapo Obi Mikel angeshika mpira, mashabiki walikuwa wanamzoea sana. ilikuwa hivyo hivyo kwa Victor Moses wa Liverpool.

Staa wao mwingine ni Adane Girma anayekipiga St George. Wameweka imani kubwa kwake ingawa anacheza nyumbani. Wameweka imani kubwa kwake kuliko Watanzania tulivyoweka imani kwa John Bocco.