England yapigwa nyumbani
LONDON, ENGLAND. MICHUANO ya UEFA Nations League iliendelea jana ambapo timu ya Taifa ya England ikiwa nyumbani ilikubali kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa Denmark katika mchezo uliopitwa katika dimba la Wembley.
Matokeo hayo yanaifanya England kushuka katika msimamo wa kundi B ambapo sasa inashika nafasi ya tatu ikiwa imepoteza mchezo mmoja, sare moja na kushinda mechi mbili ikiwa na jumla ya alama saba, huku Denmark ikipanda hadi nafasi ya pili ikiwa na alama saba pia.
Kocha wa England, Gareth Southgate alisema moja ya sababu ambazo ziliwafanya kupoteza mchezo huo ni kadi nyekundi ya mapema aliyopata beki wake Harry Maguire dakika 31.
"Ilikuwa ngumu kucheza na wachezaji kumi, mipango yetu mingi iliharibika, lakini nipongeze kile kilichofanywa na safu ya ulinzi kwa kuwa ilizua kwa umakini mkubwa, Grealish hakucheza kwa sababu nilihitaji kasi zaidi hasa katika eneo la pembeni,"alisema.
Mchezo mwingine mkali ulikuwa kati ya Italia na Uholanzi ambao ulimalizika kwa sare ya bao 1-1, ambapo lile la Italia lilifungwa na Lorenzo Pellegrini na lile la Uholanzi likafungwa na Donny van de Beek.
Matokeo ya mechi nyingine
Poland 3 - 0 Bosnia and Herzegovina
Iceland 1-2 Ubelgiji
Croatia 1 - 2 Ufaransa
Ureno 3 - 0 Sweden
Norway 1 - 0 Northern Ireland
Romania 0 - 1 Austria
Scotland 1 - 0 Czech Republic
Slovakia 2 - 3 Israel
Russia 0 - 0 Hungary
Uturuki 2 - 2 Serbia
Finland 1 - 0 Ireland
Bulgaria 0 - 1 Wales
Estonia 1 - 1 Armenia
North Macedonia 1 - 1 Georgia
Ugiriki 0 - 0 Kosovo
Moldova 0 - 4 Slovenia
Lithuania 0 - 0 Albania
Belarus 2 - 0 Kazakhstan