DStv yaleta Maisha Magic Movies Channel

Mambo hayajawahi kupungua ndani ya DStv ambapo kila uchoa burudani mpya huibuka kwenye chaneli maarufu za DStv.

Katika muendelezo huo, wale washabiki wa filamu za hapa nyumbani na Afrika mashariki, sasa wanachekelea baada ya DStv kuanza kuonyesha chaneli mpya ya Maisha Magic Movie – chaneli ambayo ni mahususi kwa filamu za Afrika Mashariki.

Chaneli hiyo iliyoanza kurindima ndani ya DStv kwa wiki moja sasa imejizolea umaarufu mkubwa kwa kutokana na kuwa na tamthilia kabambe kutoka Tanzania, Kenya na Uganda.

Maisha Magic Movies ni DStv Chaneli 141 na ni chaneli inayoonekana saa 24 kwa siku kwa wateja wote wa vifurushi vya DStv Premium, DStv Compact Plus na DStv Compact.  

Akizungumzia chaneli hii mpya, Mkuu wa Masoko wa MultiCHoice Tanzania Ronald Shelukindo amesema kuwa MulotiChoice imeamua kuiingiza chaneli hiyo kwa wateja wa DStv ili kukata kiu yao ya kutaka kuwoa na chaneli mahususi kwa filamu za hapa nyumbani nan chi zinazotuzunguka. Amesema kuwa chaneli hii ni ulingo muhimu kwa wazalishaji filamu wetu hapa nchini kwani wataweza kujipima na wenzao wa hapa Afrika Mashariki na hivyo kuongeza ushindani na ubora wa filamu zetu.

Kuongezwa kwa Chaneli hii kunamaanisha kuwa sasa DStv itachukua filamu nyingi zaidi kutoka hapa Tanzania kwa sababu uwanda wa kuonyesha filamu hizo umeongezeka. Kwa msingi huo, hii ni fursa kubwa kwa wazalisha filamu hapa nchini kuongeza uzalishaji na ubora wa kazi zao kwani zina fursa ya kuonyeshwa kwenye chaneli hiyo mpya.

Baadhi ya tamthilia na filamu maarufu zitakazokuwepo ni pamoja na: -

  • 94 Terror
  • Damu Moja
  • Freedom Movie
  • Kizingo
  • Kutu
  • Mume Mzee
  • Sangita
  • The Torture
  • Worlds Tofauti


Cha kufurahisha zaidi ni kwamba chaneli hii pia inapatikana kwenye app ya DStv Now, hivyo mteja anaweza kufurahia chaneli hii popote alipo wakati wowote kwa kutumia huduma ya DStv Now.

Chaneli hii ni ingizo jipya ndani ya DStv linaloakisi dhamira ya MultiChoice kuhakikisha kuwa wateja wa DStv wanapata vipindi na maudhui mengi nay a kuburudisha muda wote. Hii inawaongezea wateja wigo wa kuchagua kipindi na maudhui wanayoyataka wakati wowote.