Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Djuma anakuja na mashine Yanga, Makambo mambo safi

Muktasari:

BEKI matata wa DR Congo, Djuma Shabani amemshawishi straika, Fiston Mayele kukubali kutua Jangwani lakini kumbe hata dili la Heritier Makambo ni suala la muda tu.

BEKI matata wa DR Congo, Djuma Shabani amemshawishi straika, Fiston Mayele kukubali kutua Jangwani lakini kumbe hata dili la Heritier Makambo ni suala la muda tu.

Mayele ambaye akiwa na AS Vita msimu uliopita alitupia mabao 13 na kuwa mfungaji namba mbili kwenye ligi ngumu ya DR Congo ameliambia Mwanaspoti kwamba tayari amemalizana na Kocha Nabi Mohammed na anachosubiri ni kukamilishiwa ishu zake na viongozi na kuambiwa siku ya kuja.

Staa huyo ameliambia Mwanaspoti kwa njia ya simu kwamba uwepo wa Djuma ndani ya Yanga umemshawishi kwa kiasi kikubwa kukubali ofa yao lakini hata Wakongomani wenzie, Mukoko Tonombe na Tuisila Kisinda. Anasema kwamba mastaa hao wamemshawishi kuwa Yanga ni sehemu sahihi ya kung’ara.

“Kocha Nabi ameniambia kwamba anataka nije hapo nimeongea naye sana kwasasa nasubiri simu ya viongozi wao tu tumalizie, hiyo ni timu nzuri, nasikia taarifa nyingi nzuri za maisha ya hapo,” alisema Mayele ambaye ni miongoni mwa wachezaji wazoefu wa kuamua mechi DR Congo.

“Kunipata mimi ni kutokana na wao kuwasajili Djuma, Mukoko na Tuisila. Hawa ni marafiki zangu sana, tumecheza nao hapa AS Vita kwa wakati tofauti, timu ya namna hiyo utagundua kwamba inataka mafanikio.

“Huwa naongea nao sana, wananiambia kwamba wananisubiri nije hapo, najua watu wa hapo wanataka mtu anayejua kufunga, maneno ambayo hata kocha (Nabi) ameniambia pia,” aliongeza.

“Sina wasiwasi na kazi yangu. Najua kufunga. Hapo kuna viungo wazuri sana ambao tukisaidiana kwa pamoja ni rahisi kufanikiwa. Nafurahi pia kuona timu itakuwa inashiriki mashindano ya Afrika,” alisema.


ISHU YA MAKAMBO

Mwanaspoti linafahmu kwamba kama Mayele atakuja basi kuna uwezekano mkubwa kule mbele atacheza sambamba na Heritier Makambo.

Yanga inafanya mambo kimyakimya katika dili la kumrudisha Makambo ambaye aliwahi kuwa mfungaji bora wa timu hiyo kabla ya kuuzwa Horoya ya Guinea ambao hata hivyo wameshindwa kumtumia na kung’aa.

Makambo ameshacheki na Yanga na wameshakubaliana na anachosubiri ni hatua tu ya kusitishiwa mkataba na Horoya AC ambao ni mabingwa wa Guinea kwa msimu wa nne mfululizo ili aitumie nafasi hiyo kupiga pesa ya Yanga kirahisi katika dau la usajili.

Mashabiki wa Yanga wanamtaka Makambo lakini pia presha hiyo imeongezeka kutokana na baadhi ya vigogo Yanga kutaka Mkongomani huyo arejeshwe.