Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Diarra uso kwa uso tena na Percy Tau AFCON 2023


Kipa namba moja wa Yanga Djigui Diarra ameanza kwenye kikosi cha kwanza cha timu ya Taifa ya Mali ambacho kitaivaa Afrika Kusini usiku huu.

Diarra anakutana tena na mshambuliaji wa Al Ahly, Percy Tau atakayeipeperusha bendera ya Afrika Kusini katika Uwanja wa uwanja wa Amadou Gon Coulibaly unaobeba mashabiki 20,000.

Wawili hao walikutana katika mechi ya hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika, iliyomalizika kwa sare ya 1-1 katikaUwanja wa Mkapa.

Percy amechezea Afrika Kusini mechi 42 na akifunga mabao 15 huku Diarra akicheza mechi 53 bila kuruhusu bao.

Yanga ipo kundi D ikiwa nafasi ya pili na pointi tano katika mechi nne huku Al Ahly akiongoza akiwa napointi tano na kiporo cha mechi moja na nafasi ya tatu ni CR Belouizdad pointi nne sawa Medeama ya Ghana.