Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Dar City, Tausi Royals zatibua mambo BDL

Muktasari:

  • Dar City inayoongoza ligi kwa upande wa wanaume ikiwa na pointi 33 katika mchezo uliopigwa juzi iliifumua Vijana 'City Bulls' kwa pointi 70-63, huku Tausi Royals ikiifunga Pazi Queens kwa pointi 59-52 upande wa wanawake.

TIMU ya Dar City na Tausi Royals zimedhirisha ubora    katika Ligi ya Kikapu ya Mkoa wa Dar es Salaam (BDL), baada ya kushinda mechi zilizopigwa kwenye Uwanja wa Donbosco, Osterbay, huku zikitibua mipango ya timu shindani.

Dar City inayoongoza ligi kwa upande wa wanaume ikiwa na pointi 33 katika mchezo uliopigwa juzi iliifumua Vijana 'City Bulls' kwa pointi 70-63, huku Tausi Royals ikiifunga Pazi Queens kwa pointi 59-52 upande wa wanawake.

Kipigo kwa Vijana ni kama kimetibua mambo kwa wakongwe hao ambao wanalazimika kupambana kujipanga ili kurejea na kasi ya aina yake kama wanataka kuendeleza ubora na ubabe wa miaka iliyopita.

Kwa upande wake, Tausi Royals ambayo ni timu ngeni katika ligi kwenye  mchezo dhidi ya Pazi Queens iliongoza katika robo ya kwanza kwa pointi 16-14, 16-20, 17-7 na 10-11. Hata hivyo, licha ya Pazi Queens kupoteza mchezo ilionyesha kiwango bora katika robo ya pili na ya tatu.

Kwa upande wafungaji Juliana Sambwe wa Tausi Royals aliongoza akifunga pointi 14 akifuatiwa na Amina Kaswa aliyefunga nane, ilhali upande wa Pazi Queens alikuwa   Jesca Mbowe aliyefunga pointi 17 akifutiwa na Maria  Boniventura aliyetupia pointi 10

Katika mchezo wa Dar City na Vijana, wababe Dar City  waliongoza robo ya kwanza kwa pointi 19-16, 22-21, 17-12, 14-14.

Akiuzngumzia mchezo huo, Mohamed Mbwana, kocha wa Dar City alisema pamoja na ushindani uliojitokeza, lakini vijana wake walifuata maelekezo ya benchi la ufundi na kufanikiwa kushinda.