Dar City kuachia kikosi kabla ya Mei 8

Muktasari:
- Mbwana aliliambia Mwanaspoti, wachezaji wapya na wa zamani walioongezewa mikataba nao watatangazwa siku hiyo.
KOCHA Mkuu wa Dar City, Mohamed Mbwana amesema atatangaza kikosi kitakachoshiriki Ligi ya Kikapu Mkoa wa Dar es Salaam (BDL), kabla ya kufungwa dirisha la usajili Mei 8.
Mbwana aliliambia Mwanaspoti, wachezaji wapya na wa zamani walioongezewa mikataba nao watatangazwa siku hiyo.
Hata hivyo, hakutaka kudokeza majina ya wachezaji wapya na kusisitiza yatatangazwa kabla ya tarehe 8.
“Sisi usajili wetu tunafanya kwa umakini mkubwa, hatumsajiri mchezaji na baadaye anaondoka,” alisema Mbwana.
Dar City ilifungwa na JKT mwaka jana katika robo fainali kwa michezo 3-1, katika Uwanja wa Donbosco Oysterbay Ratiba iliyotolewa na kamishina wa ufundi na mashindano Haleluya Kavalambi, imeonyesha timu ya Dar City itacheza na Pazi Mei 15. Huku mchezo wa ufunguzi Ligi ya mkoa wa Dar es Salaam (BDL) itakuwa Mei 10, ni kati ya bingwa mtetezi wa ligi hiyo JKT na UDSM Outsiders.
Kwa upande wa wanawake DB Liones, bingwa mtetezi, atacheza na Vijana Quuens, na michezo yote itachezwa katika Uwanja wa Donbosco Upanga.
Dalili ya Dar City kufanya vizuri katika Ligi ya kikapu ya BDL mwaka huu, ni jinsi walivyoongeza uzoefu zaidi katika mashindano ya kumbukumbu ya mauaji ya Kimbari Rwanda.
Katika mashindano hayo ilifungwa na timu ngumu ya APR kwa pointi 81-68, katika nusu fainali iliyofanyika katika Uwanja wa Petit gymnasium, Rwanda.