Coastal Union wakwepa kuingia vyumbani Nyamagana, wavalia nje.

Wednesday July 21 2021
coastal pic
By Mgongo Kaitira

Kikosi cha Coastal Union ya jijini Tanga kimegoma kuingia katika vyumba vya kubadilishia nguo kwenye Uwanja wa Nyamagana, Mwanza badala yake wachezaji wakiongozwa na benchi la ufundi la timu hiyo wamevalia nje chini ya jukwaa la kurushi matangazo ya mchezo huo.

Baada ya kukamilisha kuvaa kikosi hicho kimeelekea moja kwa moja uwanjani na kukaa katika eneo lao kabla ya kuanza kupasha misuli.
Coastal Union wanajiandaa kuivaa Pamba SC katika mchezo wa Play Off utakaochezwa leo saa 10 jioni kwenye uwanja ww Nyanagana, jijini hapa.

Wagosi hao wa Kaya ambao wamewasili jijini hapa asubuhi kwa ndege, waliingia uwanja wa Nyamagana saa 8:45 alasiri kisha kuzunguka uwanja wakigoma kuingia vyumbani katika hali inayoonekana kuwa ni kukwepa hujuma.

Kikosi cha Coastal Union kilikuwa cha kwanza kuingia uwanjani kupasha dakika nane baadae wenyeji Pamba SC nao wakaingia kwa stairi ya kuzinguka uwanja kupitia kwenye kona ya kibendera cha lango la Kaskazini Mashariki mwa uwanja huo.

Advertisement