Clara kuwania tuzo CAF

Mshambuliaji wa klabu ya Yanga Princess na timu ya taifa ya Tanzania chini ya Umri wa miaka 17 'Serengeti Girls', Clara Luvanga ameorodheshwa kwenye orodha ya wachezaji wanaowania tuzo ya mchezaji bora chipukizi wa mwaka katika tuzo za CAF 2022 Kwa upande wa Wanawake.

Tuzo hizo zinazotolewa na shirikisho la mpira wa miguu barani Afrika (CAF), zinatarajiwa kufanyika Jijini Rabat nchini Morocco Julai 21, zina mjumuisho wa vinyang'anyiro vingi ikiwemo hicho cha mchezaji bora wakike kijana.

Clara alionyesha kiwango bora kwenye michuano ya kuwania kufuzu kombe la Dunia mwaka huu ambapo alimaliza akiwa kinara wa mabao  akiweka kambani mara 10.

Mbali ya kuwa mfungaji bora Clara aliisaidia Serengeti Girls kufuzu kucheza Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza katika historia.

Kwenye orodha hiyo pia yupo mchezaji wa Uganda anayecheza soka la kulipwa nchini Khazakhstan Fauzia Najjemba.