Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

City Bulls yageuka shamba la bibi

Muktasari:

  • Hali hiyo imeifanya timu hiyo ishindwe kuonyesha makali katika Ligi ya Kikapu Mkoa wa Dar es Salaam (BDL), kama ilivyozoeleka miaka mingi nyuma.

TIMU ya kikapu ya Vijana maarufu kama City Bulls imegeuka kuwa sehemu ambayo wachezaji wake wanachukuliwa bila na timu zingine hivyo kuwa sawa na akademi inayoibua wanamichezo na kisha wanaondoka.

Hali hiyo imeifanya timu hiyo ishindwe kuonyesha makali katika Ligi ya Kikapu Mkoa wa Dar es Salaam (BDL), kama ilivyozoeleka miaka mingi nyuma.

Msimu huu City Bulls iliyowahi kuwa bingwa wa BDL 2019, imeonyesha kushindwa kufurukuta kutokana na usajili ilioufanya kutoka kikosi chake cha pili, tofauti na timu zingine zinazoshiriki ligi hiyo zilizosajili wachezaji kutoka nje ya nchi na wale wenye uwezo mkubwa wa ndani ya nchi.

Hata hivyo, City Bulls imeonyesha ingepata mafanikio endapo wachezaji iliowakuza wangebaki kuichezea timu hiyo wakiwamo ni Jonas Mushi aliyetimkia Stein Warriors, Baraka Sabibi na Ally Mustafa wanaokipiga JKT kwa sasa huku Ally Faraji akiitumikia Dar City. Wengine waliong’ara katika timu hiyo miaka michache iliyopita ni Cosmas Ndege aliyepo UDSM Outsiders, Jorvin Ngowi na Rahim Ramadhani anayeitumikia KIUT.

Wachezaji hao enzi wakiwa City Bulls waliifanya itishe na kuongopwa na timu pinzani kutokana na ubora wao katika kila eneo la uwanja walipokuwa wakicheza.

Katika Ligi ya Kikapu Dar es Salaam mwaka jana, City Bulls ilishika nafasi sita ikiwa na pointi 44 - nafasi ambayo ilifanya icheze robo fainali na mwaka huu hadi sasa iko katika nafasi ya nane ikiwa na alama 12, huku Dar City ikiongoza kwa pointi 16.

Katika mashin-dano hayo City Bulls imebakiwa na mechi dhidi ya Mgulani JKT, Chui, Mchenga Star, Pazi, KIUT, UDSM Outsiders na Srelio huku baadhi ya michezo iliyocheza ilizifunga Kurasini Heat kwa pointi 91-54, Polisi 78-58, Savio 70-50 na kisha kupoteza kwa kufungwa na ABC 48-37, JKT 56-44, Dar City 79-41 na Stein Warriors

John Bandie, mmoja wa viongozi wa timu hiyo alidai timu shiriki zac ligi hiyo zimekuwa zinachukua wachezaji kutoka timu yao mara kwa mara na kwamba kuondoka kwa wachezaji hao kunatokana na timu hiyo kushindwa kuwekeana nao mikataba.