Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Chirwa bado haamini kilichomkuta Ligi Kuu msimu huu

Muktasari:

  • Chirwa aliyetua nchini msimu wa 2016/17 kuitumikia Yanga kutoka FC Platnum ya Zimbabwe kisha kupita Azam, Namungo, Ihefu, Kagera Sugar na KenGold, amefunga mabao mawili tu msimu huu akiifungia Kagera Sugar bao moja na KenGold kafunga bao moja.

MSHAMBULIAJI wa zamani wa Yanga, Obrey Chirwa bado haamini alichokutana nacho msimu huu wa Ligi Kuu Bara akisema ni mgumu kwake kutokana na kucheza timu mbili ngumu tofauti na zote kuwa katika nafasi zisizo nzuri, ikiwamo kushuka daraja akiwa na KenGold iliyomsajili wakati wa dirisha dogo.

Chirwa aliyetua nchini msimu wa 2016/17 kuitumikia Yanga kutoka FC Platnum ya Zimbabwe kisha kupita Azam, Namungo, Ihefu, Kagera Sugar na KenGold, amefunga mabao mawili tu msimu huu akiifungia Kagera Sugar bao moja na KenGold kafunga bao moja.

Nyota huyo akiwa kati ya wachezaji walioshuka na KenGold, aliliambia Mwanaspoti, hajawa na msimu mzuri kutokana na kushindwa kuzisaidia timu zote alizozitumikia msimu huu.

“Hauwezi kuwa msimu mzuri kwangu kwani timu zote nilizozitumikia hazina matokeo mazuri, nilianza na Kagera ambayo hata hivyo pia haipo pazuri pia na sasa KenGold tumeshindwa kuibakiza Ligi Kuu,” alisema Chirwa na kuongeza;

“Huu ni msimu dume kwangu kati ya misimu yote niliyocheza soka hapa Tanzania, nakiri kuwa sikuwa bora ndio maana nimeshindwa kuzipambania, lakini ligi ni ngumu msimu huu tofauti na misimu iliyopita kwani kila msimu mambo yanabadilika.”

Chirwa alisema KenGold ilishindwa kuchanga karata zake vizuri mzunguko wa kwanza ndio sababu iliyowaangusha anaamini walichokifanya dirisha dogo kingefanyika mwanzo wa msimu wasingerudi walipotoka.

“Ukiangalia mabadiliko yaliyofanywa katika dirisha dogo kwa viongozi kuongeza nguvu ya wachezaji wazoefu kuna kitu kimefanyika, lakini hakijaweza kuongeza nguvu kutokana na matokeo mabaya ya mzunguko wa kwanza lakini naamini wamejifunza kutokana na makosa.”