Chikupe atinga na mkoko mazoezini
Beki wa Yanga, Andrew Vincent 'Dante' mwenye jezi ya Yanga
Muktasari:
Baada ya mazoezi kumalizika Dante, alionekana kutokuwa na wasiwasi wowote wa kuondoka uwanjani hapo kulinganisha na wenzake waliokuwa wakitafuta namna ya kuondoka uwanjani hapo.
Dar es Salaam.Beki wa Yanga, Andrew Vincent 'Dante' alikuwa mazoezini leo asubuhi na timu hiyo kwenye Uwanja Uhuru huku nje ya uwanja akiwa amepaki gari yake aina ya Toyota IST.
Baada ya mazoezi kumalizika Dante, alionekana kutokuwa na wasiwasi wowote wa kuondoka uwanjani hapo kulinganisha na wenzake waliokuwa wakitafuta namna ya kuondoka uwanjani hapo.
MCL Digital lilimshuhudia beki huyo akipanda katika gari yake aina ya IST, alipoona mwandishi alitaka kujificha,lakini alishindwa kufanya hivyo na kujikuta akipigwa picha asizozitarajia.
Kiungo Papy Tshishimbi alifika uwanjani hapo akiwa na gari aina ya Ford Ranger, alikuwa akiendeshwa, wakati Ibrahim Ajib naye alikuwa na gari yake aina ya IST rangi nyeupe.
Katika mazoezi ya klabu hiyo Chikupe alionekana kupata namba moja kwa moja katika kikosi cha kwanza baada ya kuendelea kuwepo katika kikosi cha Yanga ambacho kimekuwa kikicheza mechi za kirafiki mfululizo.
Yanga inaendelea kufanya mazoezi katika uwanja wa Uhuru bila Kuwa na kocha wao George Lwandamina aliyeondoka nchini baada ya kufiwa na baba yake mzazi, pia kikosi hicho kimewakosa nyota wake watano Kelvin Yondani, Emmanuel Martin, Ramadhan Kabwili, Gadiel Michael waliokuwa katika kikosi cha timu ya taifa. Pamoja na majeruhi Beno Kakolanya, Geoffrey Mwashiuya, Baruani Yahya, Obrey Chirwa na Amis Tambwe.