Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Chanongo, Mwamita watua Prisons

Chanongo Pict
Chanongo Pict

Muktasari:

  • Msimu uliopita Prisons haikuwa na mwanzo mzuri wa ligi chini ya aliyekuwa kocha wake, Fredi Felix 'Minziro' kabla ya kumtema na kumpa kazi, Ahamd Ally aliyeonesha ubora.

WAKATI Tanzania Prisons ikianza kambi yake jijini Dar es Salaam kujiandaa na Ligi Kuu msimu ujao, benchi la ufundi na uongozi wa timu hiyo umeonesha matumaini makubwa kwa usajili walioufanya.

Msimu uliopita Prisons haikuwa na mwanzo mzuri wa ligi chini ya aliyekuwa kocha wake, Fredi Felix 'Minziro' kabla ya kumtema na kumpa kazi, Ahamd Ally aliyeonesha ubora.

Hata hivyo,  msimu ujao wa 2024/25, Maafande hao watakuwa chini ya Kocha Mkuu, Mbwana Makata aliyetokea Pamba Jiji baada ya kuwapndisha Ligi Kuu na ilikuwa ianze kambi jana Jumapili jijini humo.

Timu hiyo tayari imemalizana na nyota saba wakiwa ni Haruna Chanongo, Seleman Boban, Oscar Mwajanga, Meshack Mwamita, Sebusebu Samson, Aboubakari Ngalema na Ismail Ally.

Meneja wa timu hiyo, Raulian Mpalile alisema wameamua kuweka kambi yao Dar es Salaam ili kupata utulivu na mechi nyingi za kirafiki kutokana na wenzao wengi kuwa huko.

Alisema wanatarajia kukaa huko kwa mwezi mmoja kabla ya kurejea makao makuu jijini Mbeya tayari kusubiri ratiba ya Ligi Kuu na kwamba tayari ripoti ya kocha Makata imefanyiwa kazi.

"Kule Dar es Salaam tutapata utulivu, mechi nyingi za kirafiki kutokana na timu nyingi za Ligi Kuu kuwa kule, tutatumia siku 30 na matarajio yetu ni kufanya vizuri msimu ujao"

"Kwa sasa kikosi ni kama kimekamilika, japokuwa hatujamaliza usajili, tunachofanya ni utekelezaji wa mapendekezo ya kocha mkuu na hadi kufungwa dirisha tutaweka wazi nani katoka au kuingia”  alisema Mpalile.

Kwa upande wake Makata alisema matarajio yake ni kufanya vizuri kama alivyowahi kufanya alipoiongoza timu hiyo kwa misimu miwili tofauti akieleza kuwa anataka soka la kasi na ushindani.

"Ligi Kuu naifahamu vyema, tutajipanga kiushindani kuhakikisha Prisons inacheza kwa ubora wake, hakuna kitu kipya kwakuwa nimewahi kufanya nao kazi kwa mafanikio"  alisema Kocha huyo.