Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Championship kazi inaendelea

VITA ya kupanda Ligi Kuu Bara kwa timu za Ligi ya Championship inaendelea leo kwa michezo saba kupigwa wikiendi katika viwanja tofauti huku pia kukiwa na presha ya kushuka daraja ikizidi kupanda miongoni mwa timu zinazoshiriki.

Mechi zinazopigwa leo Jumamosi, Ndanda itakuwa wenyeji wa Pan Africans kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mtwara, huku JKT Tanzania itaialika African Sports na Kitayosce itamenyana na Mashujaa kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, Tabora.

Mechi nyingine leo ni ya kinara DTB yenye pointi 49 itakwaruzana na Transit Camp, Mwadui na Fountain Gate zitakuwa na vita yao mjini Shinyanga na Ihefu na KenGold zitakuwa kwenye vita nzito ya Mbeya Derby, jijini humo.

Makocha wa timu zote wametambiana, lakini kocha wa Ihefu inayoshika nafasi ya pili na pointi 47, Zubery Katwila alisema; “Tumejiandaa vyema kuhakikisha tunaondoka na pointi tatu, licha ya kuwaheshimu mpinzani.”

DTB na Ihefu ndizo zipo kwenye nafasi nzuri ya kupanda daraja, huku Gwambina na Lyon zikiwa mkiani zikipambana kuepuka kushuika daraja. Gwambina itavaana na Pamba leo katika mechi ya Mwanza Derby.