Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Chama, Morrison habari nyingine

KIUNGO wa zamani wa Simba, Mohamed ‘Mo’ Ibrahim amewachungulia uwanjani Clatous Chama na Bernard Morrison wanaokipiga Msimbazi na kukiri jamaa wana madini miguuni mwao na soka lao ni darasa kwa wachezaji wengine nchini.

Mo anayekipiga kwa sasa JKT Tanzania, alisema kuna vitu vingi vinavyomvutia Ligi Kuu Bara, ikiwemo aina ya uchezaji wa Chama na Morrison wakiwa kwenye kiwango cha juu, wanajua kutumia akili kuibeba timu.

“Kuna wachezaji wengi wanaojua mpira, ila mwenye kipaji anaona kipaji mwenzake, Chama na Morrison wanaujua mpira na ni rahisi mchezaji mwingine kufurahia wanachokifanya nje ya ushindani.” alisema Mo Ibrahim na kuongeza;

“Chama anatumia akili kufanya kazi yake, beki akiwa mzembe anaweza akaingia mkenge wa kupishana na mpira, vivyo hivyo kwa Morrison, ni fundi wa kutengeneza faulo zinazoisaidia timu yake kufaidika inapokuwa inakwama kwenda mbele,” alisema Mo Ibrahim aliyewahi pia kuichezea Mtibwa Sugar.

Alisema si jambo la aibu kwa mchezaji mwingine kuiga maarifa yao kwa faida ya kuleta ushindani na soka litakalowapa raha mashabiki.

Mo alipoulizwa kilichompeleka Ligi ya Championship wakati amewahi kupata nafasi kwenye timu mbalimbali za Ligi Kuu, alijibu; “Maisha ya soka yana mambo mengi zaidi ya yale yanayoonekana uwanjani. Kwa ufupi nimeamua kubadilisha mazingira mwakani nitarejea.”

Chama amerejea Msimbazi kutoka RS Berkane ya Morocco na tayari ameshafunga mabao matano na kuasisti mara nne katika Ligi Kuu Bara na katika michuano ya Kombe la Shirikisho (ASFC).

Wakati Mo Ibrahim, akifurahishwa na vipaji vya Chama na Morrison, alimsikisha mchezaji wa zamani wa Simba, Zamoyoni Mogella kuona madini ya mguu wake yameshindwa kumpa utajiri.

“Mo Ibrahim ni kati ya wachezaji wenye vipaji vikubwa nchini kama Ibrahim Ajibu, ila sijui kwa nini hawakuweka akili zao kupigania pesa,” alisema Mogella.