Chama asimamisha kwa muda mkutano wa Simba

Sunday November 21 2021
chama pic
By Imani Makongoro

Dar es Salaam. Kiungo wa Berkane ya Morocco, Cletous Chama amesimamisha kwa muda hotuba ya Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi ya Simba, Salim Abdallah 'Try Again' kwenye mkutano mkuu wa klabu hiyo.

Wanachama walilipuka kwa furaha wakati Try Again alipowaeleza kumsajili mchezaji yoyote wanayemtaka baada ya mwekezaji wa klabu hiyo, Mo Dewji kumhakikishia mzigo upo.

try PIC\

Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi ya Simba, Salim Abdallah 'Try Again' alipokuwa akizungumza na wanachama wa klabu hiyo leo katika mkutano mkuu wa Simba.

"Tutamleta yeyote, sijui awe Chama au nani, amesema Try Again na kushangiliwa kwa nguvu na wanachama wengine wakisimama na kutoa maneno ya kujisifu, hali iliyosababisha Try Again kusimama kwa sekunde kadhaa kusubiri wanachama wanalize kushangilia.

Kabla ya kumtaja Chama aliyeuzwa na klabu hiyo, Try Again alisema bodi ya Wakurugenzi imempa urais wa heshima Mo Dewji kwenye klabu hiyo kutokana na namna aluvyojitoa ndani ya klabu.

"Amenihakikishia pesa ipo, tutasajili yeyote tunayemtaka," amesisitiza Try Again kwenye mkutano huo unaoendelea jijini Da es Salaam.

Advertisement
Advertisement