Cannavaro amtaka Ngassa Yanga
Muktasari:
- Cannavaro alisema amemfuatilia Ngassa katika michezo yake mitatu ya ligi pamoja na mechi ya hisani ya kuchangia elimu ulioandaliwa na mshambuliaji wa kimataifa Mbwana Samata amegundua bado anauwezo wa kuisaidia timu.
Dar es Salaam. Nahodha wa Yanga, Nadir Haroub 'Cannavaro' amesema anatamani kuona mshambuliaji wa zamani wa klabu hiyo Mrisho Ngassa arudi kundini.
Cannavaro alisema amemfuatilia Ngassa katika michezo yake mitatu ya ligi pamoja na mechi ya hisani ya kuchangia elimu ulioandaliwa na mshambuliaji wa kimataifa Mbwana Samata amegundua bado anauwezo wa kuisaidia timu.
Alisema Ngassa ni mchezaji mzuri na amefanya mambo mengi mazuri katika klabu ya Yanga hivyo naamini endapo viongozi watafanya kweli kumrudisha ataweza kuisaidia timu kwani bado anauwezo wa kucheza na kufanya vizuri.
"Ngassa pamoja na kushindwa kuonyesha uwezo katika timu alizoenda kucheza mimi bado naamini ni bora kwasababu anakipaji na ameshindwa kufanya vyema kutokana na kukutana na wachezaji ambao hawaendani na kasi yake," alisema Cannavaro.