Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mwamnyeto aona mwanga Yanga

Muktasari:

  • Yanga ni bingwa mara nne mfululizo wa Ligi Kuu Bara kuanzia msimu wa 2021-2022 hadi 2024-2025 na msimu unaoendelea ipo kileleni mwa msimamo kwa pointi 63 baada ya kucheza mechi 26, imeshinda 19, sare sita na imepoteza moja dhidi ya Dodoma Jiji, jambo ambalo Mwamnyeto analiona bado wana nafasi ya kuchukua kwa mara ya tano.

NAHODHA wa Yanga, Bakari Mwamnyeto amesema ushindi walioupata dhidi ya Mashujaa wa mabao 2-0 umezidi kuwaongezea morali ya kupambana na kuyasogelea malengo ya kutetea ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu.

Yanga ni bingwa mara nne mfululizo wa Ligi Kuu Bara kuanzia msimu wa 2021-2022 hadi 2024-2025 na msimu unaoendelea ipo kileleni mwa msimamo kwa pointi 63 baada ya kucheza mechi 26, imeshinda 19, sare sita na imepoteza moja dhidi ya Dodoma Jiji, jambo ambalo Mwamnyeto analiona bado wana nafasi ya kuchukua kwa mara ya tano.

Chini yao kuna Simba yenye pointi 61, tofauti zikiwa ni pointi mbili pekee, huku pia Azam ikisogelea vita hiyo kwa pointi 55 ikiwa nafasi ya tatu.

“Natambua mechi nne zilizosalia siyo nyepesi, lakini kadri tunavyoshinda kama tulivyoshinda dhidi ya Mashujaa ndivyo tunavyozidi kusogea karibu na malengo yetu, jambo la msingi naendelea kuwasisitiza mashabiki walianza na sisi msimu kwa nguvu na wamalize na sisi kwa nguvu ileile,” alisema Mwamnyeto na kuongeza;

“Kazi yetu wachezaji ni kuhakikisha tunawapa mashabiki furaha, ikitokea matokeo hayajawa mazuri basi inakuwa ni bahati mbaya, hivyo tunazidi kujipanga na kujiweka sawa ili tumalize kwa ushindi mechi zilizosalia.”

Yanga imebakiza mechi dhidi ya dhidi ya Fountain Gate, Azam, TRA United na JKT Tanzania, ambazo Mwamnyeto alisisitiza zitakuwa ngumu na wanahitaji kupambana ili kuzivuna pointi 12 zitakazoamua klabu hiyo kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu.

Mwamnyeto msimu huu ana mabao mawili Ligi Kuu Bara, aliyofunga dhidi ya Simba, Mei 3, 2026 kwenye Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo katika sare ya 2-2, kisha akafunga dhidi ya Mashujaa kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika, Kigoma, Yanga ikishinda 2-0.