CAF yaomba radhi baada ya Berkane kususia mechi

Muktasari:

  • Timu hiyo kutoka nchini Morocco iliamua kuondoka uwanjani muda mfupi kabla ya mechi hiyo dhidi ya USMAlger, baada ya mamlaka nchini Algeria kuizuia kutumia jezi zao zenye bendera ya Morocco inayojumuisha eneo lenye mgogoro wa kisiasa.

Shirikisho la Soka Afrika (CAF) limeomba radhi wadau wa soka baada ya mechi ya kwanza ya nusu fainali ya mashindano ya Kombe la Shirikisho kutofanyika baada ya klabu ya RS Berkane kugoma kucheza jana Jumapili.

Timu hiyo kutoka nchini Morocco iliamua kuondoka uwanjani muda mfupi kabla ya mechi hiyo dhidi ya USMAlger, baada ya mamlaka nchini Algeria kuizuia kutumia jezi zao zenye bendera ya Morocco inayojumuisha eneo lenye mgogoro wa kisiasa.

Awali, CAF iliagiza mamlaka nchini Algeria iwarejeshee RS Berkane jezi hizo, lakini timu ilipofika kwenye vyumba vya kubadilishia nguo haikuzikuta na ndipo ikaamua kugeuza na kuondoka uwanjani.

Katika taarifa iliyowekwa kwenye tovuti ya CAF imesema suala hilo litapelekwa kwenye chombo kinachohusika kwa ajili ya uamuzi na kuomba radhi kwa mashabiki.