Bocco mfungaji bora VPL

Sunday July 18 2021
bocco pic
By Thomas Ng'itu

ACHANA na kombe ambalo Simba wamechukua huku wakiwa  na pointi 83, ishu kubwa ilikuwa kwenye upande wa wafungaji bora  msimu huu baada ya washambuliaji wa timu hiyo kufungana kwa mabao.

Mabao mawili aliyofunga Mugalu katika ushindi wa 4-0 dhidi ya Namungo yalimfanya mchezaji huyo kufikisha mabao 15 sawa na mshambuliaji mwenzake wa Simba, John Bocco.

Lakini Bocco alikata mzizi wa fitina dakika 90+baada ya kufunga bao la penalti ambayo yeye mwenyewe ameisababisha baada ya kufanyiwa madhambi na Stephen Duah.

Baada ya penalti kutokea beki Shomari Kapombe aliuchukuw mpira na kumpa Mugalu lakini aliuchukua mpira na kuupeleka kwa nahodha wake John Bocco.

KIPINDI CHA PILI KILIVYOKUWA
Kwenye kipindi cha pili cha mchezo wa Simba dhidi ya Namungo, timu zote zilikuwa zinacheza kwa kuviziana huku kila mmoja akionyesha kuhitaji bao.

Dakika 56 Abeid Athuman wa Namungo alitaka kuipatia bao la kwanza timu hiyo baada ya kupokea pasi kutoka kwa Steven Nzigamasabo lakini shuti lake dogo lilipita pembeni ya goli.

Advertisement

Abeid alikuwa mwepesi wa kupeleka mashambulizi kupitia upande wa kushoto kwa Mohamed Hussein ‘Tshabalala’ na alikuwa akibadilishana na Shiza Kichuya aliyekuwa anacheza upande wa kulia.

Dakika 59 beki wa Namungo, Stephen Duah alionyeshewa kadi ya njano baada ya kumfanyia madhambi.

Dakika 64 beki Hamis Fakhi wa Namungo alionyeshewa  kadi ya njano baada ya kuzozana na mshambuliaji wa Simba, Cris Mugalu.

Namungo katika kipindi cha pili walionekana kuimarika tofauti na walivyokuwa wanacheza kwenye kipindi cha kwanza.

Dakika 67 Simba ilipata bao la tatu kupitia kwa Cris Mugalu baada ya Miquissone kufanyiwa  madhambi na yeye mwenyewe aliuanzisha mpira huo kwa spidi na kuingiandani ya boksi na kupiga pasi kwa Mugalu aliyeweka wavuni.

Bao hilo liliwafanya wachezaji wa Namungo wahamaki wakionyesha moira ulianzishwa kwa haraka bila kutulia, muamuzi Nassor Mwinchui alionyesha kati.

Namungo walifanya mabadiliko dakika 68 wakimtoa Hamis Halifa na kuingia Stephen Sey wakati huo huo Simba wakimtoa Rally Bwalya na kuingia John Bocco.

Mabadiliko mengine yalifanywq dakika 76 kwa upande wa Simba akitoka Ibrahim Ame na kuingia Kennedy Juma kisha dakika 86, walifanya mabadiliko ya kumtoa Clatous Chama na kuingia Hassan Dilunga.

Advertisement