Bocco ampisha Paul Peter JKT Tanzania

Muktasari:
- Peter akiwa na Dodoma Jiji aliyefunga mabao manane anaenda kuungana na Matheo Antony ambaye hakuwa na msimu mzuri kutokana na kuwa nje ya uwanja kutokana na kusumbuliwa na majeraha.
MSHAMBULIAJI wa zamani wa Dodoma Jiji, Paul Peter amejiunga na JKT Tanzania akipishana na John Bocco anayetajwa kuachwa.
Peter akiwa na Dodoma Jiji aliyefunga mabao manane anaenda kuungana na Matheo Antony ambaye hakuwa na msimu mzuri kutokana na kuwa nje ya uwanja kutokana na kusumbuliwa na majeraha.
“Ripoti ya mwalimu ilikuwa inatuhitaji tusajili mshambuliaji tuimeanza na Paul Peter ambaye tunaamini atatusaidia kutokana na uwezo aliouonyesha msimu huu akiwa na timu yake aliyomalizana nayo baada ya kumal;iza mkataba,” kilisema chanzo cha taarifa.
“Licha ya kumalizana na mshambuliaji huyo bado tuna nafasi ya kusajili kiungo mshambuliaji ambaye atakuwa na uwezo wa kufunga ili kuongeza nguvu eneo hilo ambalo msimu uliopita lilituangusha na kushindwa kufikia malengo.’’
Chanzo kilisema hawakuwa bora kwenye umaliziaji wameanza kulifanyia kazi eneo hilo, lakini wapo kwenye mchakato wa kusajili eneo la ulinzi ili kuimarisha timu na kufanya kile walichotamani kukifanya msimu huu.
“Hatukuwa bora maeneo mengi lakini ushambuliaji na ukabaji ni maeneo ambayo tunataka kusajili wachezaji wenye uwezo mkubwa ili kuendana na ushindani - kama msimu huu tumekwama hatuna maana mwisho wetu.”