Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Boban kanidhihirishia Zahera ni zaidi ya kocha

Muktasari:

Hata hivyo, mashabiki hao hao wana mengi ya kujifunza wawapo viwanjani au popote wanapotazama mchezo wa soka.

WAKATI mwingine ushabiki wa soka unahitaji taaluma ya ufundi wa soka. Mashabiki ni zaidi ya wachezaji, ni zaidi ya timu na ni sehemu ya timu.
Ni sehemu ya timu kwa sababu bila wao, timu inakosa mengi, mapato, hamasa na hata kukosolewa. Wana mchango sana kwenye timu.
Hata hivyo, mashabiki hao hao wana mengi ya kujifunza wawapo viwanjani au popote wanapotazama mchezo wa soka.
Mchezaji anapokosa bao la wazi ndani ya kisanduku cha sita, kuna la kujifunza, anapokwatuliwa au kumkwatua mwenzake, kuna unalojifunza na zaidi ya yote hata wanapotolewa nje na kuingizwa mwingine, kuna unalojifunza.
Hata hivyo, katika taaluma ya ufundi, ni kazi sana kukubaliana na mambo mengi yanayotokea uwanjani. Unaweza ukapinga kwa nini mchezaji fulani kakosa bao ndani ya kisanduku cha sita, utajiuliza kwa nini mchezaji yule anacheza nafasi ile badala ya kucheza sehemu nyingine iliyozoeleka, utapinga kila kitu kinachoonekana kutokuwa vizuri machoni kwako.
Mbaya zaidi, unaweza kuwa mtaalamu wa soka lakini bado usiwe na jicho la pili la Kung'amua vipaji halisi vya wachezaji.
Ni makocha wachache wenye uwezo huo, lakini tunatakiwa kuheshimu maamuzi ya wataalamu hasa pale timu zao zinapokuwa zikifanya vizuri.

Nimefarijika sana kuona mmoja kati ya makocha wa kigeni wamekuja na kitu tofauti nchini. Ni faraja kwa sababu tunaona wazi kuna kitu tunaendelea kujifunza kutoka kwa Kocha Mwinyi Zahera hasa kwa sisi makocha wazawa, tunashukuru amekuja na kitu tofauti msimu huu.
Ni vigumu kumlinganisha Zahera na makocha waliomtangulia George Lwandamina na Babu Hans Pluijm kwenye maeneo mengi sana uwanjani.


Kwa mfano Kocha Hans Pluijm ndiye aliyekataa kumrudisha Mrisho Ngasa baada ya kushindwa kuendelea kucheza kule Free State ya Afrika Kusini akidai atakuja kupoteza nafasi za wachezaji chipukizi.

Hata hivyom, Zahera alimkubali asajiliwe baada ya kumshuhudia akifanya yake akiwa na Ndanda FC na sasa amemrudisha kwenye kiwango kizuri cha kuridhisha na kuwa mmoja wa wachezaji muhimu kikosini.
Pili Zahera anafanya kazi kubwa ya kurudisha viwango vya wachezaji kama Ibrahim Ajibu, Feisal Salum na wengineo, pia amekuwa akipandisha viwango vya chipukizi na kuwafanya kuwa tegemezi, mfano beki wa kulia, Godfrey Paul na kiungo Maka Edward, huku chini ya Lwandamina na Hans hakuna kumbukumbu ya chipukizi aliyepandishwa na akabaki na kiwango hadi sasa.
Tatu, Zahera anavyoweza kuongea kwa uwazi kuhusu uwezo wa wachezaji uwanjani na baada ya kufanuya hivyo, utaona wachezaji hao ambao wakijirekebisha na kufanya vizuri.
Amewahi kufanya hivyo kwa Heritier Makambo, sasa amebadilika. Pia kwa Ngasa, Ibrahim Ajibu, Amis Tambwe, Thaban Kamusoko na hata Feisal Salum. Hili ni funzo kwetu makocha. Kuwa wawazi kwa wachezaji.

Hata hivyo, kingine kikubwa alichotufunza, ni uwezo wake wa kung'amua vipaji vya soka nchini.
Achana na usajili wa Ngasa, huu usajili wa wiki hii wa Haruna Moshi 'Boban' mchezaji mwenye kipaji kikubwa cha Soka hapa nchini.
Hapa imenidhihirishia kocha huyu ana jicho kali sana la pili la kung'amua kipaji cha mchezaji.
Jicho hili sidhani kama lingefanywa na kocha mzawa lingepokelewa sawa na ilivyofanyika sasa na viongozi wa Yanga.
Bila sahaka mashabiki wa soka hususan wa Yanga wamepata kigugumizi kukubali usajili huu, huku wengi wakichanganyikiwa kwa kuwa walitegemea jina jipya la mchezaji wa kigeni labda au mzawa anayewika kama kina Eliud Ambokile, Said Dilunga wa Ruvu Shooting na wengineo. Mashabiki wa Yanga kwa sasa wanachekwa na kuchanganywa na wale wenzao wa Simba wakiwatania kuwa wamesajili mkongwe.

Hata hivyo, wakubali au wakatae, Kocha Zahera ameona mbali. Kumbuka kwamba, huyu sio mzawa na hajawahi kumwona Boban kabla. Alichofanya ni kuangalia tu kipaji chake na kiwango maridhawa alichokionyesha akiwa na African Lyon.
Boban anafanya mengi na ataweza kukupa yafuatayo ndani ya uwanja. Anakwenda Yanga kwa kuwa ana kipaji na anawazidi wachezaji zaidi ya saba pale Yanga. Anza kuhesabu; Deus Kaseke, Pius Buswita, Matheo Anthony, Juma Mahadhi, Rafael Daud, Baruan Akilimali, Said Makapu na chipukizi Mhilu, Mkomola na Mussa hivyo usajili wake ni ukombozi kwenye timu.
Haruna Moshi anakwenda Yanga na kukupa kazi sahihi ya nafasi zifuatazo, kucheza kama mshambuliaji namba mbili nyuma ya mshambuliaji wa mwisho, hapa ndipo Kocha Zahera alipoweza kupatia.
Kwa muda sasa nimekuwa nikimwangalia Zahera akiwajaribu kina Matheo Anthony, Thaban Kamusoko na hata Tshishimbi na siku nyingine Rafael Daud au Pius Buswita kucheza nyuma ya Heritier Makambo au Tambwe ambao ni washambuliaji wa mwisho, hata hivyo, wameshindwa kufanya hivyo.
Kumpata Boban maana yake anakwenda kutibu moja kwa moja tatizo hilo, kwani atampa kila kitu anachotaka kutoka kwa mchezaji kama Boban.
Pia atasaidia kutibu vyema nafasi ya kiungo mshambuliaji au kiungo mchezeshaji, huku pasi zake nyingi huwa zinafika kwa usahihi katika nafasi sahihi kwa wakati sahihi na zikiwa zina faida kubwa.
Kazi itabaki kwa wamaliziaji yaani washambuliaji wa mwisho.
Hata hivyo, kikubwa cha mwisho ni kuwa Haruna kama mchezaji mzoefu atatumika sana kuwatuliza vijana pale inapotakiwa, atawashauri na kuwaelekeza wachezaji wenzake na kuifanya Yanga kuwa na utulivu mkubwa. uwanjani.