Boban? Ebu cheki a.k.a za nyota hawa!

Muktasari:
Licha ya kuwa majina na uwezo mkubwa kisoka, bado wachezaji wengi wa zamani walipewa majina yaliyoshabiana na maumbo yao ama kulinganisha na wakali wengine waliokuwa enzi hizo.
BRAZILI inatajwa kama nchi ambayo wachezaji wake wamekuwa wakiitwa kwa majina ya utani kuliko majina yao halisi, kama ilivyo kwa makoloni yao ya zamani, Msumbiji na Ureno.
Ukanda wa Afrika Mashariki na Kai, Zanzibar inatajwa ndio kinara wa nyota wake kuwa na a.k.a na utamaduni huo haukuanza leo, kwani tangu zamani imekuwa hivyo. Majina kama Wembe, Kidishi, Bwanga, Kibichwa, hadi hawa kina Fei Toto, Marcelo, Cannavaro, Mo Banka ni sehemu tu ya utamaduni huo wa nyota wa visiwa hivyo kupenda kutumia majina ya utani katika soka lao.
Hata hivyo usichojua ndani ya Tanzania Bara kuna nyota waliotikisa miaka ya nyuma hata ya hivi karibuni waliotambuliwa na a.k.a zilizowatambulisha.
Achana na kina Salum Swedi 'Kussi', Said Swedi 'Panucci', Haruna Moshi 'Boban', Idd Athuman 'Chuji' ama Mussa Hassan 'Mgosi' au Idd Seleman 'Naldo, huku nyuma kulikuwa na a.k.a zilizowabeba mastaa waliotamba kwenye soka la Tanzania.
Hapo chini ni baadhi ya wachezaji hao na a.k.a zao; Makumbi Juma 'Bongabonga' a.k.a Homa ya Jiji, Zamoyoni Mogella 'Golden Boy', Itutu Kiggi 'Road Master', Abubakar Salum 'Sure Boy', Said Sued 'Scud', Juma Mkambi 'Jenerali', Venance Mwakalukwa 'Best Maridadi' na Idd Pazi 'Father'.
Wengine waliotisha na a.k.a ni Sanifu Lazaro 'Tingisha', Salum Kabunda 'Ninja', Celestine Mbunga 'Sikinde'Job Ayoub 'Kwasakwasa', Said Mwamba 'Kizota', Frank Kassanga 'Bwalya', Jamhuri Kihwelo 'Julio', George Lucas 'Gazza', Ally Malilo 'Loketo' na Deo Njohole 'OCD'.
Wapo pia kina Mwanamtwa Kihwelo 'Dally Kimoko', Willy Martin 'Gari Kubwa' a.k.a Power Iranda', Rajab Rashid 'Double R', Abdallah Seleman 'Kaburu', Rajab Rashid 'Msingida', Abeid Mziba 'Tekelo' Edward Chumila 'Edo Boy', Razack Yusuf 'Careca' na David Mwakalebela 'MP'.
Kadhalika kuna Mohammed Mwameja 'Tanzania One', Mohammed 'Tostao', Mohammed Bakar 'Tall', Hamis Gaga 'Gagarino', Method Mogella 'Fundi', Daud Salum 'Bruce Lee', Idd Seleman 'Meya' a.k.a Nyigu, Salum Mwinyimkuu 'Carlos' na Peter Lupokela 'Gari Kubwa'.
Pia wamo Bakar Malima 'Jembe Ulaya', John Makelele 'ZigZag', Malota Soma 'Ball Jugller', Samli Ayoub 'Beki Mstaarabu', Mohammed Hussein 'Mmachinga', Madaraka Seleman 'Mzee wa Kiminyio', Abbas Dilunga 'Sungura', Maulid Dilunga 'Mexico' na Kitwana Manara 'Popat'.
Wengine ni, Rashid Idd 'Chama', Athuman Juma Chama 'Jogoo', Mohammed Kajole 'Machela', Boi Idd 'Wicken', Edgar Mwafongo 'Fongo', Juma Pondamali 'Mensah', Silvatus Ibrahim 'Polisi', Maalim Saleh 'Romario', James Tungaraza 'Boli Zozo', Juma Bakar 'Kidichi' na Ali Bushir 'Benitez'.
Wakali wengine ni, Omar Hussein 'Keegan', Raphael Paul 'RP', Godwin Aswile 'Scania', Yusuf Macho 'Musso', Shadrack Nsajigwa 'Fusso', Nassor Mwinyi 'Bwanga', Twaha Hamidu 'Noriega', Said Mrisho 'Zico wa Kilosa', Thomas Kipese 'Uncle Tom' na Sunday Manara 'Computer'.
Mastaa wengine ni, Joseph Kaniki 'Golota', George Kulagwa 'Best', Ezekiel Greyson 'Jujuman', Ally Yusuf 'Tigana', Athuman Abdallah 'China', Elias Michael 'Nyoka Mweusi', Leodegar Tenga 'Injinia', Leopard Mukebezi 'Tasso', Athuman Kilambo 'Ticha' na Idd Moshi 'Mnyamwezi'.
Wamo pia kina Mohammed Nyalusi 'Shilton', Said Maulid 'SMG', Muhammed Mwarami "Shilton', Mao Mkami 'Ball Dancer', Victor Costa 'Nyumba', Steven Mapunda 'Garrincha', Abdul Ramadhani 'Mashine', Bakar Idd 'Beka Joe', Juma Burhan 'Kankoko' na Isihaka Hassan 'Chukwu'.
Wakali wengine ni Hussein Masha 'Smart Boy', Mohmmed Chopa 'Bob', Juma Limonga 'Stoper', Hamad Hilika 'Double H', Ally Nassor 'Kibichwa', Rashid Mohammed 'Tall', Hassan Abdallah 'Wembe', Khalid Ngome 'Bitebo', Sunday Juma 'Pikipiki', Sabri Ramadhani 'China', Mohammed Rishard 'Adolph', Hashim Kambi 'Ramsey' na Abdallah Kibadeni 'King Mputa'.