Biashara zadorora kwa Mkapa, ulinzi ukiimarishwa

Saturday September 25 2021
taifa pic1
By Lilian Mukulu

WAFANYA biashara njee ya Uwanja wa Benjamin Mkapa wamelalamikia bishara zao kudorora kutokana na kuwepo kwa mashabiki wachache waliokuja kutazama mechi ya Ngao ya Jamii utakaozikutanisha Simba na Yanga.

Akizungumza na Mwanaspoti Steven Joseph ambae anauza jezi amesema kutokana na bei za tiketi kuwa juu imefanya watu wachache wajitokeze uwanjani

“Kwa kweli biashara leo imekuwa ngumu kwani mashabiki waliokuja uwanjani kutazama mchezo huu ni wachache na sababu kubwa ni bei za tiketi kuingia uwanjani ni kubwa sana wengi waliozoea kuingia kwa Sh5000 ila kwa sasa ni Sh10,000” amesema Steven Joseph.

Pia Anna Juma ambae ni mfanyabiashara wa chakula njee ya uwanja huo amesema biashara leo ni ngumu sana kwani muda kama huu katika mechi zinazokutanisha Simba na Yanga chakula huwa kinaishia.

“Leo hali sio nzuri vyakula ni vingi sana mara nyingi katika mechi zinazowakutanisha Simba na Yanga mida kama hii chakula ndio tunamalizia ila leo chakula bado kingi ila tunaendelea kujipa imani kwani mechi ni saa kumi na moja jioni” amesema Anna

Ulinzi kamili gado kwa Mkapa

Advertisement

Polisi wengi wameonekana wakiimarisha ulinzi maeneo yote yanayozunguka uwanja wa Benjamin Mkapa Dar ea Salaam.

Kutokana na usalama katika uwanja huu kuna askari wasiopungua 200 katika mageti yote ya uwanja wa Benjamin Mkapa na Uhuru.

Pia barabara ya Taifa kuelekea DUCE imefungwa ikiruhusu wale tu wanaoingia uwanjani kuangalia mtanange wa watani hao.

Advertisement