Bet Pawa kuwasaidia Watanzania 20 kutimiza ndoto zao awamu ya pili ya 'Dream Maker'

Dar es Salaam. Kampuni ya michezo ya kubahatisha ya Bet Pawa Tanzania, leo imezindua awamu ya pili ya programu yake ya kuwasaidia Watanzania wenye mawazo chanya kutimiza ndoto zao inayojulikana kama ‘ Dream Maker’.Kupitia awamu ya pili ya programu hiyo, jumla ya Watanzania 20 wenye mawazo ya miradi yenye uwezo wa ku badilisha maisha yao na jamii inayowazunguka, watashikwa mkono na Bet Pawa na hivyo kutimiza ndoto zao.

Akiongea wakati wa uzinduzi wa msimu wa pili, meneja masoko wa Bet Pawa Tanzania, Borah Ndanyungu alisema programu hiyo itahusisha mikoa mitatu ambayo ni Lindi, Mtwara na Ruvuma.“Watu watakaokutana na basi maalum la Dream Maker watakaribishwa kupanda na kujaza form pamoja na kurekodi video kuhusu ndoto zao. Wengine ambao hawatapata fursa ya kukutana na basi, wanaweza kufanya hivyo popote pale walipo na kutuma kwa njia ya mtandao kwa kutumia hastag #bet PawaDreamMaker,” alifafanua
Kwa mujibu wa Bet Pawa Tanzania, msimu wa kwanza wa Dream Maker uliofanyika Septemba 2021, uliwezesha ndoto za Watanzania 13 kutimizwa. Ndoto hizo ni pamoja na ujenzi wa nyumba mpya, viwanja vya michezo ufunguzi wa biashara mpya ambazo pia zi metengeneza ajira kwa jamii inayozizunguka. Mwaka huu, jumla ya miradi 20 itapata ufadhili.

Borah alieleza kuwa fursa ipo wazi kwa kila Mtanzania mwenye umri wa miaka 18 na kuendelea na kuwataka wote wenye mawazo ya miradi kujitokeza na kuyawasilisha kwa Bet Pawa.
“Tunafanya ubashiri kuwa rafiki zaidi kwa kuwapa watu fursa ya ku bashiri kwa dau dogo na kushinda kiku bwa kisha kutimiza ndoto zao. Hata hivyo, katika programu hii ya Dream Maker, huhitaji kubashiri kabisa kwa kuwa ni ya kila mtu mwenye umri wa miaka 18 au zaidi. Tueleze ndoto yako bila kujali ukubwa wake na sisi tutakusaidia ku itimiza na kukufanya kuwa mmoja kati ya wanufaika 20 wa msimu wa pili,” alifafanua Borah
Aliongeza kuwa Bet Pawa itatembelea mikoa hiyo mitatu na magari ya matangazo yatakuwa yakihamasisha watu kujitokeza na kuelezea ndoto zao.
Zoezi hililitafanyika katika mikoa tofauti tofauti kila msimu hadi litakapomaliza nchi nzima.
“Lengo la Bet Pawa Tanzania ni kutoa fursa kwa kila Mtanzania kutimiza ndoto yake,” aliongeza.