Beki Yanga mguu sawa kwa Ligi Kuu

Muktasari:

Furaha imerejea kwa beki wa Yanga, Adeyum Saleh kutokana na Ligi Kuu Bara,kutangazwa itaendelea, hivyo anaona burudani itaendelea kwake na mashabiki.

BEKI wa Yanga, Adeyum Saleh (24),amefurahia kurejea kazini baada ya kukaa nje  tangu Machi 16,  serikali ilipokuwa imetangaza kusitisha shughuli za mikusanyiko.
Amesema licha ya soka kuwa kazi lakini pia ni kati ya burudani anayoipenda, hivyo kurejea kazini ni kama kumtoa kifungoni.
Kitu anachokizingatia baada ya kurejea kazini ni umakini kama wanavyoelekeza watalamu wa afya,amesisitiza yupo makini ili kujilinda na kulinda wengine.
"Mungu atuepushie ugonjwa wa covid 19, ili amani iendelee kutawala kama ilivyokuwa mwanzo, binafsi nimefurahi kurejea mzigoni,"
Ameongeza kuwa"Pamoja na kwamba ligi ilisimama lakini aliendelea na programu ya mazoezi hivyo anaamini ataonyesha ushindani kama kawaida kuhakikisha anakuwa msaada ndani ya kikosi cha Yanga,"amesema.
Beki huyo ambaye ni msimu wake wa kwanza kucheza Yanga, akitokea JKT Tanzania amesema anaamini timu yake itafanya maajabu ya kuwastajabisha wapinzani wao katika ligi.
"Kwa mazoezi ambayo tumeyafanya, yametuweka fiti kwamba kila mechi kwetu itakuwa kama fainali ya kutoa kipigo cha kwa wapinzani,kwani bado tuna nafasi ya kutwaa ubingwa,"amesema.