Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Beki Yanga ajifua ufukweni

Muktasari:

  •  Beki huyo ameachwa na klabu ya Yanga msimu huu na sasa anajiandaa kwa ajili ya usajili wa dirisha dogo

Dar es Salaam. Beki wa zamani wa Yanga, Oscar Joshua amerudi Dar es Salaam na sasa anapiga tizi la maana kwenye ufukwe wa Coco ikiwa ni maandalizi ya safari yake ya nje na inadaiwa ni Afrika Kusini.

Oscar ambaye alikuwa kwao Mwanza kwa ajili ya kukamilisha zoezi la kufunga ndoa, amerudi Dar es Salaam kwa kishindo na kutokomea huko bichi.

"Nataka kurudi uwanjani sasa, ndiyo maana nimeamua kuingia mafichoni ili safari yangu itakapokamilika iwe rahisi. Kuna mawakala nazungumza nao lakini wiki hii ndiyo naweza kuwa na uhakika ni wapi, ila nchi inaweza kuwa ni Afrika Kusini," alisema Oscar.

"Lakini, kama dili langu litachelewa hadi mzunguko wa pili, naweza kusaini timu za hapa kwa miezi sita kwa ajili ya kujiweka fiti zaidi na baada ya hapo, nitaondoka."

Oscar aliachwa na Yanga baada ya mkataba wake kumalizika msimu uliopita na hivi karibuni alifunga ndoa jijini Mwanza na mama watoto wake.