Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Beki Yanga aandika historia

UNAMKUMBUKA yule beki wa kushoto aliyetamba kwenye kikosi cha Yanga na Taifa Stars kutokana na kucheza soka la nguvu, Oscar Joshua ‘OJ’? Bado hajastaafu soka lakini anaandaa kitabu ambacho kitahusu maisha yake yote ya mpira lengo likiwa ni kuwapa motisha vijana.

Oscar kwa sasa ameweka kambi na kufanya mazoezi yake binafsi katika fukwe za Coco kwani muda wowote kuanzia Januari mwakani, ataondoka kwenda Afrika Kusini au China.

“Unajua kwa kipindi chote wakati nacheza, kuanzia Toto, Ruvu Shooting, Yanga, timu ya Mkoa wa Mwanza na Taifa Stars kila mechi na tukio langu nimeliandika kwenye kitabu cha kumbukumbu zangu.  Mbali kumbukumbu hizo,  kwa sababu najua mambo mengi katika mpira wa Tanzania namna ya kuuboresha na kinachoudidimiza, katika kitabu nitaandika yote,” alisema Oscar  na kufafanua, kitabu hicho anategemea kukikamilisha mwishoni mwa mwaka ujao atakaporudi nchini.

AWEKA KAMBI COCO BEACH

Katika kuimarisha afya yake na atakapokwenda kucheza nje mambo yake yawe mazuri, Oscar ameanza kujifua kwa nguvu zote kwenye fukwe za Coco.

“Muda wowote kuanzia Januari natarajia kwenda nje, nimeshafanya mipango na timu za Afrika Kusini na China kutakapokuwa sawa ndiko nitakwenda. Unajua kama mpira wa hapa nchini nimeshacheza sana, lengo la kwenda nje ni kuweka historia na kukamilisha malengo niliyokuwa nimeyakusudia kwa kipindi kirefu.”