Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Beki JKT Tanzania anogewa na vigogo

BEKI Pict

Muktasari:

  • Bakiri alikuwa sehemu ya kikosi kilichoituliza Yanga kwa kuambulia suluhu Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo na mechi dhidi ya Simba wakikubali kichapo cha bao 1-0.

BAADA ya kucheza mechi mbili dhidi ya Simba na Yanga, beki wa JKT Tanzania, Karim Bakiri amesema timu hizo kongwe zina nyota wengi bora ambao wanaufanya mpira kuwa mwepesi wakikutana nazo tofauti na akicheza na timu za madaraja ya kawaida ambazo hufanya jasho liwatoke.

Bakiri alikuwa sehemu ya kikosi kilichoituliza Yanga kwa kuambulia suluhu Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo na mechi dhidi ya Simba wakikubali kichapo cha bao 1-0.

Akizungumza na Mwanaspoti, Bakiri alisema huwa anafurahi kucheza mechi kubwa kwa sababu anacheza kwa kujiamini na kutumia akili, sio nguvu kutokana na kukutana na wachezaji wazuri wenye vipaji vikubwa huwa wanacheza kwa nafasi, tofauti na akicheza na timu za madaraja ya chini huwa hawaelewi wanacheza mfumo gani.

“Hakuna kazi kucheza na Simba na Yanga na maandalizi yanakuwa ya kawaida tu, nazingatia maelezo ya kocha na ndicho ninachokifanya uwanjani. Nafikiri urahisi wake unatokana na kucheza na wachezaji ambao wana vipaji vikubwa na na wanacheza kwa mfumo tofauti na mechi nyingine,” alisema Bakiri.

Akizungumzia mechi ijayo ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho utakaopigwa Mei 18 dhidi Yanga, alisema haitakuwa rahisi kwa vile ni  mtoano hivyo dakika 90 ndizo zitakazoamua nani bora zaidi ya mwingine.

“Baada ya suluhu sasa kuna dakika nyingine 90 ngumu ambazo ndizo zitakazoamua nani bora kutokana na jkutafutwa mshindi na sio kugawana pointi naamini huu utakuwa mchezo mgumu na wa ushindani mkubwa,” alisema Bakiri na kuongeza;

“Timu ambayo itajiandaa vizuri ndio itakayoibuka na ushindi na naamini hautakuwa mchezo rahisi kutokana na kial timu kuhitaji matokeo ili iweze kusonga mbele kwenye michuano hiyo na sisi tukitaka taji ili kupata nafasi ya uwakilishi kimataifa.”

JKT imefuzu nusu fainali kwa kuitoa Pamba Jiji wakati Yanga iliitoa Stand Unied, huku nusu fainali ya pili itapigwa Mei 31 kati ya Simba na Singiga Black Stars zilizozitoa Mbeya City na Kagera Sugar mtawalia.